Unaweza kubadilisha utambulisho wako mara mbili ndani ya siku 14. Ukifanya hivyo, tunahifadhi utambulisho wako wa awali kwa siku 14 endapo utapenda kuutumia tena. Kwa kipindi hiki cha siku 14, URL ya utambulisho wako wa awali na URL uliyobadilisha zote zitafanya kazi. Baadaye, utambulisho utapatikana kwa watumiaji wengine ili wauchague kuwa utambulisho wao. Pata maelezo zaidi kuhusu utambulisho kwenye YouTube.
Kuangalia au kubadilisha utambulisho wako
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Kubadilisha upendavyo
Wasifu.
- Chini ya Utambulisho, unaweza kuangalia au kubadilisha URL ya utambulisho wako.
- Ukibadilisha utambulisho wako, bofya CHAPISHA ili uuthibitishe.
Kumbuka: Iwapo utambulisho unaopendelea haupatikani, unaweza kujaribu kuweka nukta, namba au mistari chini. Iwapo umejaribu kufanya hivyo na bado haupatikani, basi ni kwa kuwa chaneli nyingine inautumia au haujafuata mwongozo wetu wa majina ya utambulisho.
Kuficha utambulisho wako
Iwapo ungependa kuficha utambulisho wako, unaweza kufuta au kuficha chaneli yako.