Ikiwa wewe ni mtayarishi wa video, unaweza kutumia zana ya klipu za video kukata kwa urahisi sehemu zinazoshirikisha katika video zako ndefu kwenye YouTube na uzichapishe papo hapo kama video tofauti. Zana hii inapatikana kwa watayarishi wote na katika video zote.
Kutayarisha klipu za video
- Kwenye Studio ya YouTube, chagua Maudhui
Video
.
- Fungua video iliyopo ambayo ungependa kutumia kutayarisha klipu za video
.
- Chagua Klipu kisha ubofye “Tayarisha klipu ya video” katika kona ya juu kulia.
- Chagua sehemu ya video iliyopo ambayo ungependa kudondoa iwe klipu mpya ya video. Kuna njia 3 za kufanya hivi:
- Chaguo la kwanza: Chagua maandishi katika manukuu ambayo ungependa kutumia kwenye klipu ya video yako kisha ubofye “Thibitisha uchaguzi.” Utaona sehemu uliyochagua imeangaziwa katika kihariri cha video.
- Chaguo la pili: Bofya neno katika manukuu ambalo ungependa liwe la kwanza kwenye klipu video yako, bofya “Weka liwe Mwanzo,” bofya neno katika manukuu ambalo ungependa liwe la mwisho kisha ubofye “Weka liwe mwisho.”
- Chaguo la tatu: Weka muhuri wa wakati ambako ungependa klipu ya video yako ianze, bofya kitufe cha “Weka Mwanzo” kwenye kihariri kisha uweke muhuri wa wakati wa kumaliza au usogeze aikoni ya kuburuta katika kihariri hadi sehemu ambapo ungependa kumalizia klipu ya video yako kisha ubofye “Weka mwisho.”
- Ukiridhika na klipu ya video hiyo, chagua Andaa Rasimu katika kona ya juu kulia. Utaweza kukagua kwanza klipu ya video hiyo katika kidirisha cha kupakia.
- Ili uweke video ya utangulizi na ya utamatishaji kwenye klipu ya video yako, bofya kitufe cha “Weka utangulizi au utamatishaji” kisha uchague video inayotimiza masharti
.
- Kamillisha kidirisha cha kupakia jinsi ambavyo ungefanya katika video nyingine yoyote.
Kutayarisha klipu za video kwa kutumia mapendekezo yaliyotayarishwa kwa AI
Klipu unazopendekezewa na AI hupata mihtasari muhimu kutoka kwenye video za podikasti yako. Utaona mapendekezo haya unapofungua zana ya klipu za video. Unaweza pia kuangalia muhtasari uliotayarishwa kwa AI ili upitie kwa urahisi manukuu ya video yako. AI hutafuta matukio yanayoweza kuchapishwa kama video mpya.
Jinsi ya kutayarisha kwa kutumia mapendekezo yaliyotayarishwa kwa AI
- Kwenye Studio ya YouTube, chagua Maudhui
Video
.
- Fungua video iliyopo ambayo ungependa kutumia kutayarisha klipu za video
.
- Kwenye menyu ya upande wa kushoto, chagua Klipu.
- Katika kona ya juu kulia, chagua Tayarisha klipu ya video.
- Angalia kila klipu unayopendekezewa kwa kuchagua jina lake.
- Si lazima: Unaweza kurekebisha sehemu za kuanzia na kuishia za klipu ukitumia manukuu au kihariri cha video.
- Katika kona ya juu kulia, bofya Andaa rasimu.
- Kumbuka: Ukitumia klipu uliyopendekezewa bila kufanya mabadiliko, unaweza kuona jina unalopendekezewa. Ukirekebisha muda wa kuanza au kuisha kwa klipu, utahitaji kuandika jina.
- Kamillisha kidirisha cha kupakia jinsi ambavyo ungefanya katika video nyingine yoyote.
Kupata klipu ya video uliyotayarisha
Klipu za video ni kama video yoyote kwenye YouTube. Ili upate klipu za video unazotayarisha, nenda kwenye Maudhui Video
. Pia, unaweza kupata klipu zote za video zilizotayarishwa kutokana na video mahususi kwa kwenda katika ukurasa wa Maelezo wa video hiyo kisha ubofye kichupo cha Klipu.