Sasisha mipangilio ya faragha ya video yako ili udhibiti sehemu ambapo video yako inaweza kuonekana na wanaoweza kuitazama.
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Elekeza kwenye video ambayo ungependa kusasisha. Ili uone video unazopakia moja kwa moja, chagua kichupo cha Mubashara.
- Bofya vishale vya chini kwenye "Uonekanaji" kisha uchague Ya Umma, Ya Faragha au Haijaorodheshwa.
- Hifadhi.
Kumbuka: Mipangilio chaguomsingi ya faragha ya video kwa watayarishi walio na umri wa kati ya miaka 13 hadi 17 huwa ya faragha. Iwapo una umri usiopungua miaka 18, mipangilio chaguomsingi ya faragha ya video hubainishwa kuwa ya umma. Kila mtu anaweza kubadilisha mipangilio hii ili kufanya video yake iwe ya umma, ya faragha au haijaorodheshwa.
What are video privacy settings on YouTube?
Kuhusu mipangilio ya faragha
Video za ummaVideo na orodha za kucheza za faragha zinaweza tu kutazamwa nawe na mtu yeyote unayemchagua. Video zako za faragha hazitaonekana katika kichupo cha Video cha ukurasa wa kwanza wa chaneli yako. Hazitaonekana pia katika matokeo ya utafutaji kwenye YouTube. Mifumo ya YouTube pamoja na wahakiki wanadamu wanaweza kukagua video za faragha ili kubaini hakimiliki, ufaafu wa kuwekwa matangazo na hatua nyingine za kuzuia matumizi mabaya.
Ili utume video ya faragha:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
- Bofya kisanduku cha Uonekanaji kisha uchague Tuma kwa faragha.
- Weka barua pepe ambako ungependa kutuma video yako, kisha uchague HIFADHI.
Maoni hayapatikani kwenye video za faragha. Iwapo ungependa kuruhusu maoni kwenye video ambayo haipatikani hadharani, badilisha mipangilio ya faragha iwe haijaorodheshwa.
Video na orodha za kucheza ambazo hazijaorodheshwa zinaweza kutazamwa na kutumwa na mtu yeyote aliye na kiungo. Video zako ambazo hazijaorodheshwa hazitaonekana katika kichupo cha Video cha ukurasa wa kwanza wa chaneli yako. Hazitaonekana katika matokeo ya utafutaji kwenye YouTube isipokuwa mtu aongeze video yako ambayo haijaorodheshwa kwenye orodha ya video hadharani.
Unaweza kutuma URL ya video ambayo haijaorodheshwa. Wale unaowatumia video hiyo hawahitaji Akaunti ya Google ili kuona video hiyo. Mtu yeyote aliye na kiungo anaweza pia kuituma tena.
Kipengele | Faragha | Haijaorodheshwa | Ya Umma |
---|---|---|---|
Unaweza kutuma URL | Hapana | Ndiyo | Ndiyo |
Inaweza kuwekwa katika sehemu ya chaneli | Hapana | Ndiyo | Ndiyo |
Inaweza kuonekana katika utafutaji, video zinazohusiana na mapendekezo | Hapana | Hapana | Ndiyo |
Imechapishwa kwenye chaneli yako | Hapana | Hapana | Ndiyo |
Inaonekana katika mipasho ya Wanaofuatilia | Hapana | Hapana | Ndiyo |
Unaweza kutoa maoni kuihusu | Hapana | Ndiyo | Ndiyo |
Inaweza kuonekana katika orodha ya video inayoonekana hadharani | Hapana | Ndiyo | Ndiyo |