Kuboresha Machapisho Yako kwa Kutumia Vipengele Vipya ✨
Kuna zana mbalimbali unazoweza kutumia kukusaidia kujieleza na kuwasiliana na hadhira yako ukitumia machapisho ya maandishi na ya picha. Kwa sasa zana hizi zinapatikana tu katika Kiingereza kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi.
Unaweza kutumia zana zinazotumia AI ili zikusaidie kutayarisha na kuhariri machapisho yako. Pata maelezo zaidi kuhusu mwongozo wetu wa kutayarisha maudhui ukitumia AI zalishi kwenye YouTube.
Kumbuka:
- Maudhui yote kwenye YouTube, ikiwa ni pamoja na maudhui yaliyotayarishwa kwa AI, ni sharti yafuate Mwongozo wetu wa Jumuiya. Ili kukusaidia uelewe sera zetu, tumeweka ulinzi katika zana zetu za akiliunde unaolenga kukusaidia ufuate Mwongozo wetu wa Jumuiya ili uepuke kutayarisha maudhui yasiyofaa. Huenda tusikubali vidokezo vinavyokiuka sera zetu au vinavyoangazia mada nyeti.
- Watayarishi wanaotunga au kuhariri chapisho wakitumia zana za akiliunde (AI) zalishi za YouTube, hawahitaji kuchukua hatua za ziada kufumbua matumizi ya maudhui sanisi au yaliyobadilishwa. Zana itafumbua kiotomatiki matumizi ya AI kwa niaba ya watayarishi. Pata maelezo zaidi kuhusu kufumbua matumizi ya maudhui sanisi au yaliyobadilishwa.
Kubadilisha maandishi upendavyo ukitumia zana ya kuhariri
Zana ya kuhariri hutumia AI zalishi kupendekeza maneno, toni au marekebisho ya urefu wa machapisho yako.
- Kwenye programu ya YouTube, gusa Buni
Chapisho.
- Katika kisanduku cha maandishi, andika chapisho lako. Unahitaji kuandika angalau herufi 6.
- Gusa
ili ujaribu chaguo tofauti.
- Kumbuka: Unaweza kutuma maoni yako kwa kugusa alama ya sijaipenda
na unaweza kutueleza zaidi.
- Kumbuka: Unaweza kutuma maoni yako kwa kugusa alama ya sijaipenda
- Gusa Tumia.
Kubuni picha ukitumia Dream Screen
- Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana tu nchini Australia, Kanada, Nyuzilandi na Marekani.
- Kwenye iOS, kipengele hiki kinapatikana tu katika iPhone.
Dream Screen ni kipengele cha AI zalishi kinachofanyiwa majaribio kinachokuwezesha kutekeleza mawazo yako. Kinabuni picha za kipekee kulingana na vidokezo vya maandishi unavyoweza kuweka kwenye machapisho yako.
- Kwenye programu ya YouTube, gusa Buni
Chapisho.
- Katika sehemu ya chini ya skrini, gusa
au
Buni picha.
- Fafanua picha ambayo ungependa kutayarisha.
- Gusa Tayarisha toleo la kukagua.
- Kumbuka: Unaweza kutuma maoni yako kwa kugusa
Je, kuna tatizo?
- Kumbuka: Unaweza kutuma maoni yako kwa kugusa
- Chagua picha ambayo ungependa kutumia.
- Gusa Tumia.
Hariri machapisho ya picha ukitumia zana inayotumia AI
Kumbuka:
- Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana tu nchini Kanada, India, Nyuzilandi na Marekani kwenye vifaa vya mkononi. Upatikanaji unaweza kubadilika katika siku zijazo.
- Ni lazima wamiliki wawe na umri wa miaka 18 au zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu ukadiriaji wa umri.
Unaweza kuhariri picha yako ya machapisho yako ukitumia zana ya kuhariri inayotumia AI.
-
Kwenye programu ya YouTube, gusa Buni
Chapisho.
-
Chagua picha:
- Kupitia toleo la kukagua matunzio
gusa Hariri
kwenye picha ambayo ungependa kubadilisha.
- Kupitia kiteua matunzio
chagua picha zako
Inayofuata.
- Kupitia toleo la kukagua matunzio
- Weka kidokezo kwenye sehemu ya maelezo katika sehemu ya chini.
- Gusa Weka kisha ukague mabadiliko. Unaweza kuendelea kuweka vidokezo ili ufanye mabadiliko zaidi.
- Kumbuka: Unaweza kutuma maoni yako kwa
au
kisha utueleze zaidi.
- Kumbuka: Unaweza kutuma maoni yako kwa
- Ukisharidhika na matokeo, gusa Hifadhi ili utekeleze mabadiliko.
- Gusa Chapisha katika sehemu ya juu kulia ili utume.
Faili ya maelezo ya C2PA
Huenda picha zilizotayarishwa kwa AI zikajumuisha faili sahihi ya maelezo ya C2PA iliyotiwa sahihi. Ukitayarisha klipu kwa kuchagua aikoni ya na utumie tena au utume maudhui unayotayarisha yaliyo na faili ya maelezo ya C2PA kwenye mfumo wa nje, mfumo huo unaweza kufikia metadata hii.
Kutuma maoni
Sawa na zana yoyote ya AI zalishi, huenda tusiwe sahihi kila wakati. Ndiyo maana tunawahimiza watayarishi wakague maudhui yote yaliyotayarishwa kwa AI kwa makini kabla ya kuyachapisha kwenye YouTube, kama vile wanavyofanya katika hali nyingine.
Ukipata matatizo na picha au maandishi yaliyobuniwa ya machapisho yako, unaweza kututumia maoni.
Tungependa ujihisi salama unapotumia YouTube. Ndiyo maana tunakuhimiza utufahamishe iwapo video au maoni kwenye tovuti yanakiuka faragha au usalama wako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kulinda utambulisho wako kwenye YouTube.