Kudhibiti maoni

Unaweza kuwaalika wadhibiti ili wasaidie kudhibiti maoni kwenye video na chaneli yako. Mtu yeyote aliye na chaneli ya YouTube anaweza kuwa mdhibiti.

Maoni kwenye YouTube: Kujibu, Kuchuja na Kudhibiti

Zana za kudhibiti maoni

Kuna njia kadhaa za kufikia zana za kudhibiti maoni kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi.

Jinsi ya Kudhibiti na Kuchuja Maoni

Kudhibiti kwenye mipangilio ya maoni

Ikiwa wewe ni mmiliki wa chaneli au mdhibiti, nenda kwenye video yoyote kisha uguse Maoni kisha Mipangilio . Hapo, unaweza kudhibiti mipangilio ya maoni ya chaneli, ikiwa ni pamoja na:

Kitendo

Mmiliki wa chaneli

Mdhibiti mkuu

Mdhibiti wa kawaida

Mipangilio ya maoni ya video

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Kuweka, kufuta au kunakili maneno yote yaliyozuiwa

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Kuwasha au kuzima kipengele cha kuzuia viungo

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Kudhibiti maoni kwenye ukurasa wa kutazama

Ikiwa wewe ni mmiliki au mdhibiti wa chaneli, gusa Zaidi kando ya maoni kwenye video ili uangalie chaguo za udhibiti. Hapo, unaweza kudhibiti maoni mahususi, ikiwa ni pamoja na:

Kitendo

Mmiliki wa chaneli

Mdhibiti mkuu

Mdhibiti wa kawaida

Kubandika au kubandua maoni

Ndiyo

Hapana

Hapana

Kufuta au kuzuia maoni

Ndiyo – Kufuta

Ndiyo – Kuzuilia

Ndiyo – Kuzuilia

Kuripoti maoni

Ndiyo

Ndiyo

Ndiyo

Kuwaongeza au kuwaondoa wadhibiti wakuu

Ndiyo

Hapana

Hapana

Kuwaongeza au kuwaondoa wadhibiti wa kawaida

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Kuongeza au kuondoa watumiaji walioidhinishwa

Ndiyo

Ndiyo

Hapana

Kuongeza au kuondoa watumiaji waliofichwa

Ndiyo

Ndiyo

Ndiyo

Kuchukua hatua kwenye maoni yaliyozuiliwa

Kwenye kichupo cha “Yaliyozuiliwa”, unaweza kuchukua hatua zifuatazo. Unaweza pia kupata chaguo hizi kwenye kichupo cha “Yaliyochapishwa” kwa kubofya Zaidi .

  • Kuidhinisha: Chagua Idhinisha ili uruhusu maoni yaonekane kwa umma.
  • Kuondoa: Chagua Ondoa ili uondoe maoni.
  • Kuripoti taka au matumizi mabaya: Chagua Ripoti ili uripoti taka au matumizi mabaya kwenye maoni. Pata maelezo zaidi kuhusu maoni taka.
  • Kumficha mtumiaji: Chagua Ficha Maps hide icon, visibility off ili umfiche mtumiaji asionekane kwenye chaneli.​ Pata maelezo zaidi kuhusu kuficha maoni ya watu mahususi.
  • Kuidhinisha kila wakati: Chaguo hili linapatikana tu kwenye kichupo cha “Yaliyochapishwa”. Ili uruhusu maoni yote ya baadaye kutoka kwa mtazamaji fulani yaidhinishwe kiotomatiki na yaonekane kwa umma, chagua Zaidi kisha Idhinisha kila wakati maoni kutoka kwa mtumiaji huyu.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, mdhibiti wa maoni anaweza kufanya mambo gani?

Hatua anazoweza kuchukua mdhibiti wa maoni hutegemea iwapo ni mdhibiti wa kawaida au mdhibiti mkuu. Wadhibiti wakuu wana chaguo zaidi zinazopatikana kuliko wadhibiti wa kawaida. Wadhibiti wa aina zote mbili wanaweza kuzuilia maoni ili uyakague.

Wadhibiti hawawezi kufikia chaneli yako kwenye Studio ya YouTube. Maoni yatazuiliwa ili uyakague kwenye foleni yako ya “Yaliyozuiliwa”. Watazamaji wengine hawataona maoni hayo isipokuwa ukiyaidhinisha.

Udhibiti wa maoni hufanya kazi kwa njia tofauti kwenye gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kukabidhi wadhibiti kwenye gumzo za moja kwa moja.

Ninawezaje kumwondoa mdhibiti wa maoni?

Unaweza kuwasimamia wadhibiti wako kwa kufuata hatua zilizo hapo juu za kumweka mdhibiti wa maoni, kisha uteue chaguo la kumwondoa.

Nini kitatokea nikitia alama kuwa maoni ni taka?

Maoni hayo yatafichwa kabisa kwenye chaneli yako. YouTube inaweza pia kukagua maoni husika na tabia ya mtoa maoni ya kuhusishwa na taka.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
1375716780884522526
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false