Ahadi ya YouTube ya kuboresha matumizi ya AI kwa kuwajibika inajumuisha kuhakikisha kuwa watayarishi pamoja na wenye hakimiliki wanaendelea kudhibiti jinsi maudhui yao yanavyotumiwa. Baadhi ya watayarishi na wenye hakimiliki wanaweza kupenda kushirikiana na kampuni za AI kusaidia kuboresha teknolojia mpya zaidi ya AI Zalishi.
Ikiwa wataamua kufanya hivyo, watayarishi na wenye hakimiliki wanaweza kuruhusu kampuni za wengine zinazounda mifumo ya AI zitumie video zao za YouTube katika mafunzo ya mfumo wa AI. Ili kufanya hivyo, wanaweza kuwasha mipangilio ya mafunzo ya wengine kisha wachague kampuni za kuruhusu.
Masharti ya maudhui
Maudhui yanatimiza masharti ya mafunzo ya wengine iwapo:
- Wenye hakimiliki husika kwenye video wanaruhusu mafunzo ya wengine.
- Mipangilio ya faragha ya video imewekwa kuwa ya umma.
- Video inatii Sheria na Masharti pamoja na Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.
Nini maana ya kuruhusu mafunzo ya wengine
Ukichagua kuwasha mipangilio ya mafunzo ya wengine, inamaanisha:
- Unachagua kwenye orodha ya kampuni za wengine ili kuruhusu au kuchagua kuruhusu kampuni zote za wengine.
- Unaruhusu kampuni za wengine ulizochagua zitumie maudhui yako kwa madhumuni ya kufunza mifumo ya AI wanayounda.
- Kwa watayarishi wanaotumia Studio ya YouTube: Maudhui yako yanajumuisha video zote zinazotimiza masharti zilizopakiwa kwenye chaneli yako.
- Kwa wenye hakimiliki wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube: Maudhui yako yanajumuisha video zote unazodai zinazotimiza masharti pamoja na video zilizo kwenye chaneli ulizounganisha. Pata maelezo zaidi.
- Hali ya ruhusa ya mafunzo ya video itapatikana kulingana na utambulisho wa video kwenye YouTube Data API ambayo ni kiolesura kinachoweza kufikiwa na umma.
- YouTube inaweza kuruhusu kampuni nyingine zifikie video zako mradi wewe na wenye hakimiliki wengine husika mmechagua kuruhusu kampuni hiyo.
Kuangalia na kubadilisha mipangilio ya mafunzo ya wengine
Kutumia Studio ya YouTube
Wamiliki wa chaneli wanaweza kuangalia na kubadilisha mipangilio ya mafunzo ya wengine wakati wowote kwenye mipangilio ya chaneli katika Studio ya YouTube.
Kutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube
Wasimamizi wanaweza kuangalia na kubadilisha mipangilio ya mafunzo ya wengine wakati wowote kwenye ukurasa wa Mipangilio katika Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube.
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)
Unaweza kuwasha au kuzima mipangilio wakati wowote. Pia unaweza kurejea wakati wowote ili ubadilishe kampuni za wengine unazoruhusu.
Kumbuka kuwa kunaweza kuwa na ucheleweshaji wa hadi siku 7 ili mabadiliko yaonekane katika kiolesura kinachoweza kufikiwa na umma (YouTube Data API).
Ukiruhusu mafunzo ya wengine, inamaanisha kuwa YouTube inaweza kuruhusu video zako zinazotimiza masharti zifikiwe na kampuni za wengine kwa madhumuni ya mafunzo ya mifumo ya AI wanayounda.
Kumbuka kuwa huenda kampuni za wengine zisitumie maudhui yako, hata ikiwa unaziruhusu.
Pia, kwa kuwa kampuni za wengine ni tofauti na YouTube au Google, hatimaye hatuwezi kudhibiti mambo ambayo kampuni ya wengine hufanya.