Iwapo unatayarisha video au Video Fupi za elimu, washirika wetu wa elimu, kama vile shule na walimu, wanaweza kuchagua kupachika maudhui yako katika nyenzo zao za mafunzo. Washirika wa elimu wakiamua kupachika maudhui yako au kutazama maudhui yako ambayo tayari yamepachikwa, huenda wakatumia Kichezaji cha Elimu. Kichezaji cha Elimu ni kichezaji kilichopachikwa kinachoboresha jinsi YouTube inavyoonyesha video katika zana za elimu.
Kulipwa kutokana na maudhui ya elimu
Washirika wetu wa elimu wanalipa ili kupata leseni ya Kichezaji cha Elimu kutoka YouTube. Kichezaji hutoa ulinzi wa ziada wa faragha kwa wanafunzi na huwapatia hali ya matumizi iliyobuniwa kwa madhumuni ya kujifunza. Kama sehemu ya matumizi hayo, kichezaji hakionyeshi matangazo. Ingawa hakuna matangazo yoyote, bado unaweza kuchuma mapato kutokana na kiwango cha muda ambacho watu wanatazama video zako kwenye kichezaji.
Ukikubali masharti ya kulipa ya Kichezaji cha Elimu, unaweza kulipwa kutokana na video zako kuchezwa kwenye Kichezaji cha Elimu, kulingana na uwiano wako wa mgawo wa muda wa kutazama wa kila mwezi katika kichezaji. Fedha hizi zinatokana na ada za leseni zinazotolewa na washirika wa elimu.
Kutia saini masharti yako ya kulipa
Kabla uanze kuchuma mapato kupitia Kichezaji cha Elimu, utahitaji kutia saini masharti ya kulipa. Ikiwa kuna uhitaji wa maudhui yako ya elimu, utapata mkataba wa kusaini.
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Chagua kichupo cha Chuma mapato.
- Kwenye Njia zaidi za kuchuma mapato, chagua Kichezaji cha Elimu.
- Chagua Anza kisha ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini.
Mikataba hutumwa kwa watayarishi wapya wanaotimiza masharti kila mwezi.
Ukishakubali masharti, yatatumika kwenye chaneli zote unazohusiana nazo na unaweza kuanza kuchuma mapato kutokana na muda wako wa kutazama wa Kichezaji cha Elimu.
Kupata mapato yako
Ukiwa na mapato yanayotokana na muda wa kutazama wa Kichezaji cha Elimu, yataonekana na kulipwa kupitia AdSense. Unaweza pia kuyaangalia kwenye Takwimu za YouTube. Mapato yanayotokana na Kichezaji cha Elimu yataonekana mara moja kila mwezi.
Kuangalia utendaji wako
Iwapo ungependa kuangalia utendaji maudhui yako ya Kichezaji cha Elimu, ikiwa ni pamoja na utazamaji na muda wa kutazama, unaweza kuangalia kwenye Takwimu za Google.
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
- Kwenye ripoti, bofya HALI YA KINA au ANGALIA ZAIDI.
- Chuja kulingana na Aina ya Kichezaji kwenye Kichezaji cha Elimu.