Kupata maelezo kuhusu mitiririko mubashara

Mitiririko mubashara hukuwezesha kutazama maudhui yanayoonyeshwa katika muda halisi kwenye YouTube. Maonyesho ya kwanza hukuwezesha kutazama video mpya pamoja na watayarishi na jumuiya zao katika muda halisi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kujiunga na mtiririko mubashara.

Kuhusu mitiririko mubashara

Ukijiunga na mtiririko mubashara, unaweza:

Mitiririko mubashara iliyoratibiwa, Maonyesho ya kwanza na mitiririko mubashara katika mkao wa mlalo haitaonyeshwa kwenye Video Fupi.

Je, ninaweza kutazama marudio ya mitiririko mubashara?

Baada ya mtiririko mubashara kukamilika, mtayarishi anaweza kuchapisha mihtasari au marudio ya mtiririko huo kwenye chaneli yake. Mihtasari na marudio huonekana kama video kwenye chaneli yake.

Gumzo la Moja kwa Moja ni nini?

Unapotazama mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza, unaweza kuwasiliana na wengine kwa kutuma ujumbe katika Gumzo la Moja kwa Moja.

  • Kipengele cha Gumzo la Moja kwa Moja kinapatikana tu kwenye kurasa za kutazama za YouTube, si kwenye vichezaji vilivyopachikwa.
  • Kumbuka kufuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube na mwongozo wa kuwa salama katika mitiririko mubashara.
  • Wakati wa mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza, unaweza kutuma hadi ujumbe 11 kwenye gumzo kila baada ya sekunde 30. Kila ujumbe haupaswi kuzidi herufi 200.
  • Herufi maalum kama vile URL au lebo za HTML hazirihusiwi kwenye Gumzo la Moja kwa Moja.
  • Baadhi ya Magumzo ya Moja kwa Moja hukupa chaguo la kuwapa motisha watayarishi kwa kuwatumia Super Chat au Super Stickers. Ukishanunua, Super Chat na Super Stickers hukuwezesha uchapishe ujumbe na vibandiko vyenye rangi ya kuvutia vilivyobandikwa wakati wa mitiririko mubashara na Maonyesho ya kwanza.

Mihtasari inayotayarishwa kwa AI ni nini?

Watazamaji wapya wanaojiunga na mtiririko mubashara wanaweza kuona muhtasari wa gumzo uliotayarishwa kwa AI. Si mitiririko yote mubashara itakuwa na muhtasari wa gumzo. Mihtasari ya gumzo inatayarishwa kwa kutumia mazungumzo ya umma kwenye Gumzo la Moja kwa Moja linaloendelea, si muhtasari wa maudhui ya mtiririko mubashara.

Kumbuka:

  • Iwapo gumzo ni la wanaofuatilia chaneli pekee, huenda usiweze kufikia vipengele vyote vya Gumzo la Moja kwa Moja.
  • Kipengele cha muhtasari uliotayarishwa kwa AI kinafanyiwa majaribio kwa sasa na kinaweza kuonyesha maelezo yasiyo sahihi, ya kukera au yasiyofaa ambayo hayawakilishi msimamo wa Google au chaneli husika. Watazamaji wanaweza kutoa maoni kwa kuweka alama ya bomba au ya hainipendezi na kutoa maoni yoyote ya ziada.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu