Katika Kituo cha Familia unaweza kuona na kudhibiti wasifu kwenye YouTube Kids na matumizi yanayosimamiwa ya vijana na vijana wako wadogo. Katika Kituo cha Familia unaweza pia kuunda wasifu mpya kwenye YouTube Kids au kuweka mipangilio ya usimamizi ya kijana wako.
Kumbuka: Ingawa huwezi kuweka mipangilio ya matumizi yanayosimamiwa ya kijana mdogo katika Kituo cha Familia, bado unaweza kuona na kudhibiti akaunti za vijana wadogo unaowasimamia kwa sasa.
Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya Kituo cha Familia vinavyopatikana kwa:
Nenda kwenye Kituo chako cha Familia
- Ingia katika YouTube kwenye kompyuta yako.
- Bofya picha yako ya wasifu .
- Bofya Mipangilio .
- Nenda chini kwenye Kituo cha Familia kisha ubofye Dhibiti wasifu wa watoto pamoja na vipengele vya vijana.