Ikiwa chaneli yako ya YouTube imedukuliwa, kwa kawaida humaanisha kuwa wadukuzi wamefanya mabadiliko ambayo hayajaidhinishwa kwenye chaneli yako na Akaunti ya Google inayohusiana. Baada ya kurejesha Akaunti yako ya Google, unaweza kuanza kusafisha chaneli yako ya YouTube ili kutendua mabadiliko ambayo hujayaidhinisha. Kuna njia mbili za kusafisha chaneli yako:
- Kutumia zana ya kusafisha katika Studio ya YouTube (inapatikana tu kwa wadhibiti na wamiliki wa chaneli)
- Kusafisha chaneli mwenyewe
Jinsi ya Kurejesha Chaneli Iliyodukuliwa
Kutumia zana ya kusafisha katika Studio ya YouTube
Zana ya kusafisha ya Studio ya YouTube huonyesha orodha ya shughuli zisizo za kawaida kwenye chaneli yako ili uweze kuzikagua zote kwa pamoja na kuamua hatua utakazochukua.
Ukishathibitisha kuwa hukufanya mabadiliko, zana hiyo hupendekeza hatua za kuchukua na inaweza kurekebisha mabadiliko hayo. Unaweza pia kukagua ruhusa za chaneli katika zana hiyo, ili uweze kuondoa ufikiaji au kufanya marekebisho haraka ikiwa inahitajika.
|
|
Hatua itakayofuata
- Tutafanya mabadiliko uliyoomba mara tu utakapotuma ukaguzi wako. Mabadiliko yatafanyika ndani ya saa kadhaa.
- Utapokea barua pepe yenye kiungo cha kufuatilia ombi lako la kusafisha.
- Ikihitajika, unaweza kurudi kwenye zana ya kusafisha na ubadilishe ukaguzi wako kabla ya tarehe iliyobainishwa kwenye barua pepe, kwa kawaida huwa siku 30 baada ya kutuma ukaguzi. Kumbuka kuwa unaweza kubadilisha mabadiliko uliyowekea alama kuwa umeyaidhinisha, lakini huwezi kutendua mabadiliko uliyowekea alama kuwa hujayaidhinisha.
Ili ukamilishe kusafisha chaneli yako:
- Katika Studio ya YouTube, angalia ukurasa wako wa Dashibodi
ili uone ikiwa ulipata maonyo yoyote mapya kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya. Iwapo ulipata, wasiliana nasi ili tuanzishe uchunguzi.
- Hakikisha kuwa maelezo yako kama vile jina la chaneli, utambulisho, picha ya wasifu na picha ya bango havijabadilishwa bila idhini yako.
- Kagua maoni mapya zaidi yaliyotolewa na chaneli yako.
- Angalia orodha, vijipicha vyako maalum na chaneli unazofuatilia.
- Kagua mipangilio ya akaunti yako ya AdSense na ya Kidhibiti Maudhui ili uhakikishe kuwa bado iko jinsi unavyoitaka.
- Chukua hatua za kulinda chaneli yako ili usaidie kuzuia isidukuliwe.
Kusafisha chaneli mwenyewe
Wakati chaneli ya YouTube imedukuliwa, mabadiliko ya mara kwa mara yanayofanywa na wadukuzi yanaweza kupatikana kwenye maudhui wanayopakia, ruhusa za chaneli pamoja na maelezo ya chaneli. Ili utendue mabadiliko yoyote ambayo hujaidhinisha:
- Chukua hatua dhidi ya upakiaji ambao haujaidhinishwa
- Ondoa watumiaji wasiojulikana
- Rejesha maelezo ya msingi na chapa ya chaneli yako
Ili uhakikishe kuwa umefanya ukaguzi wa kina kwenye chaneli yako na akaunti ya Google inayohusiana, ni muhimu uangalie iwapo kuna mabadiliko mengine ambayo huenda mdukuzi alifanya.
Kuchukua hatua dhidi ya upakiaji ambao haujaidhinishwa- Ikiwa video zilizopakiwa na mdukuzi hazina maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, maonyo ya hakimiliki au madai ya Content ID, unapaswa kuzifuta.
- Ikiwa video zilizopakiwa na mdukuzi zina madai au maonyo, wasiliana nasi ili tuanzishe uchunguzi.
-
Kwa chaneli zinazotumia Studio ya YouTube: Ondoa ufikiaji kwenye chaneli yako
-
Kwa Akaunti za Biashara: Ondoa watumiaji kwenye Akaunti yako ya Biashara
Iwapo kipengele chochote kati ya hivi kimebadilishwa, ni muhimu uvirejeshe haraka katika hali yake ya awali ili chaneli yako isisimamishwe kabisa kutokana na ukiukaji wa chapa ya biashara.
- Jina la chaneli: Sasisha jina la chaneli yako.
-
Kumbuka: Ikiwa umeshindwa kusasisha jina la chaneli yako, hakikisha kuwa tafsiri zozote zimefutwa kwanza.
-
- Utambulisho: Sasisha utambulisho wa chaneli yako.
- Picha ya wasifu: Sasisha picha ya wasifu ya chaneli yako.
- Picha ya bango: Sasisha picha ya bango ya chaneli yako.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuangalia ili uhakikishe kuwa chaneli yako na akaunti ya Google inayohusiana vimekaguliwa kwa kina:
- Angalia mipangilio ya faragha ya video zako. Huenda wadukuzi wakabadilisha mipangilio yako ya faragha ili video zako zilizopo zifichwe.
- Kagua maoni mapya zaidi yaliyotolewa na chaneli yako.
- Angalia orodha, vijipicha vyako maalum na chaneli unazofuatilia.
- Ikiwa una akaunti za AdSense na Kidhibiti Maudhui, angalia mipangilio ili kuhakikisha kuwa bado ziko jinsi unavyotaka ziwe.
- Kuwasha Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa
- Kuweka mipangilio ya Uthibitishaji wa Hatua Mbili ukitumia ufunguo wa siri
- Kuweka chaguo za mbinu za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti
Kupata usaidizi zaidi kwenye YouTube
Ikiwa wewe ni mtayarishi unayetimiza masharti (kwa mfano mtayarishi aliye kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube) na tayari umerejesha Akaunti yako ya Google, unaweza kuwasiliana na timu ya Usaidizi kwa Watayarishi ili upate usaidizi zaidi.
Ikiwa huwezi kuwasiliana na timu yetu ya Usaidizi kwa Watayarishi, pata usaidizi kutoka @TeamYouTube kwenye X.