Kwa nini YouTube ilibadilisha video zangu kuwa za faragha?

Katika hali fulani, tunapobaini shughuli za kutiliwa shaka kwenye chaneli yako, huenda tukachukua hatua ya kuweka video ziwe za faragha ikiwa tunaamini kuwa zilipakiwa na mdukuzi. Tunachukua hatua hizi ili kulinda vyema chaneli na jumuiya yako.

Ikiwa tutaweka video zako zozote ziwe za faragha, tutakuarifu kwa barua pepe. Pia, tutakuondoa kwenye akaunti yako ili kuhakikisha kuwa wewe na jumuiya yetu ya YouTube mnalindwa.

Ninapaswa kuchukua hatua gani?

Ikiwa umechapisha video hizo

Angalia video zako za faragha kabla ya kuamua ziwe au zisiwe tena za umma. Ikiwa unafikiri zinafuata Mwongozo wetu wa Jumuiya, unaweza kubadilisha video ziwe za umma.

Kumbuka: Ikiwa huwezi kubadilisha video zako ziwe za umma, huenda video yako ikawekewa alama kuwa ni ya faragha kwa sababu nyingine. Pata maelezo zaidi kuhusu video zilizowekwa kuwa za faragha kutokana na matumizi ya lebo zisizohusiana au zinazopotosha.

Ikiwa hukuchapisha video hizo

  1. Tembelea studio.youtube.com na ufute video zozote ambazo hukupakia. Hata video za faragha zinapaswa kufuata Mwongozo wa Jumuiya na hatungependa uadhibiwe kwa sababu ya maudhui ambayo hukuchapisha.
  2. Tekeleza ukaguzi wa usalama kwenye akaunti yako ya Google na uchukue hatua zozote zinazopendekezwa. Huenda vitendo vinavyopendekezwa vikajumuisha kubadilisha nenosiri lako au kuondoa vifaa vya zamani.
  3. Kagua anayeweza kufikia chaneli yako. Angalia ruhusa za chaneli ili uhakikishe kuwa hakuna watumiaji wowote wasiohitajika wanaohusishwa na akaunti yako.
  4. Angalia ikiwa mdukuzi alibadilisha kitu chochote kwenye chaneli yako, kama vile bango, viungo kwenye maelezo ya video au maoni yaliyobandikwa.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuimarisha usalama wa akaunti yako dhidi ya wadukuzi kwenye Kituo chetu cha Usalama cha Watayarishi au kwa kutembelea sehemu ya Linda akaunti yako ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8079075595781016001
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false