Kutayarisha na kudhibiti mikusanyiko ya Ununuzi kwenye YouTube

Wasaidie watazamaji wanunue kwa urahisi bidhaa zako zinazopendekezwa kulingana na mada kwa urahisi kwa kuratibu mkusanyiko wa bidhaa unazopenda. Wape watazamaji hali ya ununuzi wa nguo na bidhaa za urembo kwa kutuma mkusanyiko wa bidhaa zinazopendekezwa kwenye duka lako na ikiwa uko katika mpango wa Washirika, wape pia bidhaa unazopenda kutoka kwenye chapa nyingine.

✨NEW✨Create Custom Shopping Collections

Mikusanyiko inaweza kuonekana kwa watazamaji katika duka la chaneli yako, orodha za bidhaa na maelezo ya video. Tutaonyesha mkusanyiko wako wa hivi majuzi katika duka la chaneli yako na mkusanyiko unaofaa zaidi mtazamaji katika orodha za bidhaa na maelezo ya video.

Hakikisha kuwa unaanzisha mikusanyiko inayofuata Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Kuanzisha mkusanyiko

Tumia programu ya Studio ya YouTube ya vifaa vya mkononi  ili uanzishe mkusanyiko:

  1. Kwenye menyu ya chini, gusa Chuma mapato .
  2. Gusa Ununuzi.
  3. Kwenye “Mikusanyiko”, gusa Anzisha mkusanyiko.
  4. Chagua na upakie picha ya jalada ya mkusanyiko wako.
  5. Weka “Jina” la mkusanyiko wako kisha uweke maelezo.
  6. Gusa  Weka ili utafute bidhaa za kujumuisha katika mkusanyiko wako.
    1. Ni lazima uchague angalau bidhaa 3 ili uanzishe mkusanyiko.
    2. Unaweza kuweka hadi bidhaa 30 kwenye mkusanyiko wako.
    3. Gusa  Weka karibu na bidhaa ili uijumuishe kwenye mkusanyiko wako.
    4. Gusa na ushikilie  Sogeza karibu na bidhaa ili uihamishe juu au chini kwenye orodha. Mpangilio wa bidhaa unaoonyeshwa kwenye zana ya uteuzi ndivyo ambavyo bidhaa zako zitaonyeshwa kwa watazamaji.
    5. Gusa  Futa karibu na bidhaa ili uiondoe.
  7. Gusa Nimemaliza utakapomaliza kuweka, kuondoa na kupanga upya bidhaa zako.
  8. Kagua maelezo ya mkusanyiko wako ikijumuisha picha ya jalada, jina, maelezo na bidhaa.
  9. Gusa Chapisha.

Kudhibiti mkusanyiko

Unaweza kubadilisha mkusanyiko wako wakati wowote ukitumia programu ya Studio ya YouTube ya vifaa vya mkononi. Ili ubadilishe mkusanyiko wako:

  1. Kwenye menyu ya chini, gusa Chuma mapato .
  2. Gusa Ununuzi.
  3. Karibu na “Mikusanyiko”, gusa kisha.
  4. Gusa picha ya jalada ya mkusanyiko ambao ungependa kubadilisha.
  5. Fanya mabadiliko kwenye mkusanyiko wako.
    1. Gusa  Weka ili utafute bidhaa za kujumuisha katika mkusanyiko wako.
    2. Gusa na ushikilie  Sogeza karibu na bidhaa ili uihamishe juu au chini kwenye orodha. Mpangilio wa bidhaa unaoonyeshwa kwenye zana ya uteuzi ndivyo ambavyo bidhaa zako zitaonyeshwa kwa watazamaji.
    3. Gusa  Futa karibu na bidhaa ili uiondoe.
    4. Gusa picha yako ya jalada ili ubadilishe picha ya mkusanyiko wako.
    5. Gusa visanduku vya “Jina” au “Maelezo” ili ubadilishe jina au maelezo ya mkusanyiko wako.
  6. Gusa Chapisha.

Mkusanyiko wako wa ununuzi, ikiwa ni pamoja na kijipicha, jina, kiungo, maelezo na bidhaa zinazojumuishwa kwenye mkusanyiko, lazima zitii Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.

Ikiwa sehemu yoyote ya mkusanyiko wako inakiuka Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, mkusanyiko wako wote utaondolewa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2669607163661279478
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false