Hapa Google, tumejitolea kukupa uwazi, uwezo wa kuchagua na udhibiti wa data yako, ikiwa ni pamoja na jinsi inavyotumika katika utangazaji.
Tunawapa watumiaji wa iPhone, iPad na Apple TV uwezo wa kujijumuisha ili wapokee matangazo yaliyowekewa mapendeleo na yanayowafaa zaidi kwenye YouTube. Kidokezo kinachofuata mwongozo wa Uwazi wa Ufuatiliaji wa Programu kwenye Apple (ATT), sasa kitaonekana katika programu ya YouTube, kikikuomba uruhusu. Chaguo lako linaathiri kila mtu anayetumia kifaa hicho.
Jinsi ya kuwasha au kuzima ruhusa
Unapofungua programu ya YouTube, unaweza kupata kidokezo cha kukuomba ruhusa. Chagua iwapo ungependa kuipa programu ya YouTube ruhusa:
- Ruhusu: Ukiwasha mipangilio hii, shughuli kwenye programu hii zitaunganishwa na shughuli katika programu na tovuti zisizo za Google ili kuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo na kutoa upimaji wa matangazo. Chaguo lako litatumika kwa watumiaji wote wa programu ya YouTube kwenye kifaa ambako mipangilio imewashwa.
- Omba Programu Isifuatilie: Ikiwa hutawasha mipangilio hii, shughuli kwenye programu hii hazitaunganishwa na shughuli katika programu na tovuti zisizo za Google ili kuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo na kutoa upimaji wa matangazo. Hatua hii itafanya hali yako ya jumla ya matangazo kwenye programu hii iwekewe mapendeleo kidogo na huenda ikasababisha uone matangazo yasiyofaa sana na yanayorudiwa mara nyingi zaidi.
Mipangilio hii haiathiri kuunganishwa kwa shughuli kwenye programu na tovuti nyingine za Google na shughuli kwenye programu na tovuti zisizo za Google. Mipangilio hii pia haiathiri matumizi ya shughuli kutoka kwenye programu ya YouTube ya iOS, ya iPadOS au ya tvOS pamoja na programu na tovuti nyingine za Google ili kuwekea matangazo mapendeleo, kulingana na chaguo lako la matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye Google.
Kidokezo hakitaonyeshwa kwa watumiaji wote. Kwa mfano, watumiaji wa YouTube Premium pamoja na walio na akaunti za watoto kwenye YouTube hawataonyeshwa kidokezo.
Unaweza kwenda kwenye mipangilio ya programu ya YouTube katika kifaa chako ili ubadilishe mipangilio hii wakati wowote.