Akaunti yangu ya AdSense katika YouTube ilifungwa kutokana na chanzo cha hadhira kisicho sahihi

Mifumo yetu hukagua mara kwa mara wanaoona tangazo kwenye video ili kubaini iwapo watazamaji hao ni sahihi au si sahihi. Chanzo cha hadhira kisicho sahihi ni shughuli yoyote kwenye chaneli yako ambayo haitoki kwa mtumiaji halisi au mtumiaji aliyevutiwa kihalali. Inaweza kuwa ni pamoja na, lakini si tu njia za ulaghai, ghushi, au hata zisizokusudiwa za kuongeza mapato ya matangazo kwenye video. Vyanzo vya hadhira visivyo sahihi vinaweza kuathiri chaneli yako, hata kama huvielekezi kimakusudi. 

Tukibaini kuwa akaunti yako ya AdSense katika YouTube inahusishwa na vyanzo vya hadhira visivyo sahihi, tunaweza kufunga akaunti yako. Kufunga akaunti yako hulinda mfumo wetu kwa ajili ya watayarishi, watangazaji na watazamaji. Kwa kuendelea kulinda mifumo yetu ya utangazaji dhidi ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi, watangazaji wanaweza kuwekeza kwa uhakika kwenye YouTube, hali ambayo huwasaidia watayarishi kama wewe, kuchuma mapato kupitia maudhui yako. 

Je, akaunti yangu inaweza kurejeshwa baada ya kufungwa kwa sababu ya kuwa na chanzo cha hadhira kisicho sahihi?

Mara nyingi, mifumo yetu hufanya uamuzi sahihi kuhusu vyanzo vya hadhira visivyo sahihi. Lakini, ikiwa unahisi kuwa uamuzi huu ulifanywa kimakosa, unaweza kukata rufaa dhidi ya shughuli isiyo sahihi. Ni lazima ubainishe kwamba wewe na mtu yeyote unayemwajibikia hamkusababisha chanzo cha hadhira kisicho sahihi kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja. 

Tunapopokea rufaa yako, tutakagua kwa uangalifu maelezo tuliyopewa na kukupa uamuzi wa mwisho. Kumbuka kuwa hakuna hakikisho kwamba akaunti yako itarejeshwa. Tukishafanya uamuzi kuhusu rufaa yako, huenda rufaa za baadaye zisizingatiwe.

Ni vidokezo gani ninaweza kutumia ili kuandika rufaa itakayofanikiwa dhidi ya chanzo cha hadhira kisicho sahihi? 

  • Soma mifano hii ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi. Je, sababu yoyote kati ya hizi inahusika kwako au kwa maudhui yako? Je, huenda kuna mtu yoyote alibofya matangazo yako mara nyingi mno? Je, ulinunua wanaoona tangazo hali iliyosababisha kuongezeka kwa chanzo cha hadhira kisicho sahihi? Je, unaweza kufanya mabadiliko ya maudhui au tabia ili kuzuia chanzo cha hadhira kisicho sahihi kisitokee tena?
  • Kwenye fomu ya rufaa dhidi ya shughuli isiyo sahihi, weka anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako iliyofungwa ya AdSense katika YouTube. Kuweka barua pepe kwenye fomu hutusaidia kupata akaunti yako na kupunguza ucheleweshaji katika kuchakata rufaa yako.
  • Bainisha sababu zozote zinazoweza kusababisha vyanzo vya hadhira visivyo sahihi kwenye video zako. Pia, eleza jinsi utakavyohakikisha kuwa vyanzo vya hadhira visivyo sahihi havitajirudia tena. Toa maelezo mengi iwezekanavyo ili kufafanua ombi lako.
    • Kwa mfano, tuambie ikiwa umenunua wanaoona tangazo kutoka kwa mtu mwingine ili ukuze hadhira yako. Eleza ulivyoacha kufanya kazi na mshirika huyu mwingine, na hutafanya kazi na washirika wengine kwa lengo la kukuza chaneli katika siku zijazo.  

Akaunti yangu ilifungwa na rufaa yangu ilikataliwa. Ninaweza kujiunga tena kwenye mpango au kufungua akaunti mpya?

Tunaelewa wasiwasi wako kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya akaunti yako. Hatua zetu zimetokana na uchunguzi wa makini uliofanywa na timu yetu ya wataalamu, kwa kuzingatia maslahi ya watangazaji, watayarishi na watazamaji wetu. 

Watayarishi ambao akaunti zao zimefungwa kwa sababu ya vyanzo vya hadhira visivyo sahihi hawaruhusiwi kushiriki tena kwenye AdSense. Kwa sababu hii, watayarishi hawa hawaruhusiwi kufungua akaunti mpya.

Google inahifadhi haki ya kufunga akaunti kwa sababu yoyote, ikiwa ni pamoja na chanzo cha hadhira kisicho sahihi kutoka chanzo chochote.

Kwa nini akaunti yangu ilifungwa kwa sababu ilihusiana na akaunti nyingine iliyofungwa?

Ikiwa akaunti inayohusiana imefungwa, wataalamu wetu wamebaini kuwa akaunti yako inahatarisha watayarishi, watazamaji na watangazaji wetu.

Je, bado nitalipwa mapato yangu ya AdSense katika YouTube?

Ikiwa akaunti yako ilifungwa kwa sababu ya chanzo cha hadhira kisicho sahihi au ukiukaji wa sera zetu, unaweza kutimiza masharti ya malipo ya mwisho ya sehemu ya mapato ambayo haijatambuliwa kuwa si sahihi. Akaunti ikishafungwa, malipo yataahirishwa kwa siku 30 ili tuweze kukokotoa malipo ya mwisho (ikiwa yapo). Kufuatia kipindi hiki cha siku 30, ingia kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube ili uangalie salio lako lililobaki ambalo limetimiza masharti (ikiwa lipo) na ufanye mipango ya kupata malipo. Pesa zitakazokatwa kutoka kwenye salio lako la mwisho kwa sababu ya kuwa na chanzo cha hadhira kisicho sahihi na ukiukaji wa sera za watayarishi zitarejeshwa kwa watangazaji walioathirika panapofaa na iwezekanavyo.

Je, bado nitapata fomu za kodi za malipo ambayo nimeyapokea?

Bado tunaweza kukupa fomu ya kodi ikiwa: 

  • Tumekutumia malipo hapo awali, au 
  • Salio linalopaswa kulipwa lililosalia kwenye akaunti yako

Pata maelezo zaidi kuhusu kulipa kodi kwenye mapato yako ya AdSense katika YouTube.

Akaunti yangu ilirejeshwa. Kwa nini matangazo hayaonyeshwi kwenye tovuti, programu au video zangu?

Baada ya akaunti yako kurejeshwa, inaweza kuchukua hadi saa 48 kwa matangazo kuanza kuonyesha tena. 

Kumbuka: Huenda ukahitaji kuhusisha upya chaneli yako ya YouTube na akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio kwenye akaunti ya malipo ya AdSense katika YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1998539382552018129
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false