Matangazo kwenye YouTube huchangia kuwasaidia watayarishi unaowapenda na kuwezesha mabilioni ya watu kote duniani watumie huduma ya kutiririsha maudhui. Unapozuia matangazo ya YouTube, unakiuka Sheria na Masharti ya YouTube. Iwapo unatumia vizuia matangazo, tutakuomba uruhusu matangazo kwenye YouTube au ujisajili kwenye YouTube Premium. Ukiendelea kutumia vizuia matangazo, huenda tukakuzuia kucheza video. Ili uepuke kukatizwa, ruhusu matangazo kwenye YouTube au ujisajili kwenye YouTube Premium.
Namna ya kuruhusu matangazo kwenye YouTube
Fuata maagizo ya kiendelezi chako cha kuzuia matangazo.
AdBlock
- Kwenye kona ya juu kulia ya kiendelezi cha kivinjari chako, bofya AdBlock . Huenda ukaona nambari ndogo iliyofunika AdBlock.
- Bofya Usitekeleze kwenye kurasa za tovuti hii.
- Kwenye kidirisha cha “Usitekeleze AdBlock kwenye”, bofya Usijumuishe. Aikoni ya AdBlock hubadilika kuwa Imeruhusiwa .
- Pakia YouTube upya.
Adblock Plus
- Kwenye kona ya juu kulia ya kiendelezi cha kivinjari chako, bofya Adblock Plus . Huenda ukaona nambari ndogo iliyofunika AdBlock Plus.
- Bofya aikoni ya Kuwasha/Kuzima ili uitelezeshe kushoto.
- Ili upakie YouTube upya, bofya kitufe cha Onyesha upya.
uBlock Origin
- Kwenye kona ya juu kulia ya kiendelezi cha kivinjari chako, bofya uBlock origin . Huenda ukaona nambari ndogo iliyofunika uBlock Origin.
- Bofya aikoni ya Kuwasha/Kuzima . Aikoni itageuka kijivu kuonyesha kwamba matangazo kwenye YouTube hayazuiwi tena.
- Ili upakie YouTube upya, bofya Onyesha upya .
Vizuia matangazo vingine
- Bofya aikoni ya kiendelezi cha kizuia matangazo cha kivinjari chako. Kwa kawaida, aikoni hiyo hupatikana kwenye kona ya juu kulia ya kivinjari chako.
- Kumbuka kuwa huenda ukawa umesakinisha zaidi ya kizuia matangazo kimoja.
- Fuata maagizo ya kuzima kizuia matangazo husika kwa ajili ya YouTube. Huenda ukahitaji kuteua chaguo la menyu au kubofya kitufe.
- Pakia YouTube upya kwa kufuata maagizo au kubofya kitufe cha "Onyesha upya" au "Pakia upya" cha kivinjari chako.
Jinsi ya kuripoti tatizo
Ukiona ujumbe wa kuzima kizuia matangazo wakati huna kizuia matangazo au tayari umekizima, tuarifu. Ili uripoti tatizo hilo, nenda kwenye kona ya chini kushoto ya ujumbe huo kisha ubofye Ripoti tatizo.
Jinsi ya kudhibiti matangazo yanayoonyeshwa kwenye YouTube
Matangazo yanayocheza kwenye video au Video Fupi za YouTube unazotazama yamewekwa kulingana na mambo yanayokuvutia. Pata maelezo zaidi kuhusu matangazo yaliyo kwenye video unazotazama. Iwapo ungependa kutumia YouTube bila matangazo, huku ukiendelea kuwasaidia watayarishi unaowapenda, angalia manufaa ya uanachama wa YouTube Premium.