Kuchapisha au kuondoa vipindi katika mipasho ya RSS kwenye YouTube

Ikiwa wewe ni mtayarishi wa podikasti, unaweza kutumia Studio ya YouTube ili upakie podikasti zako kwenye YouTube kupitia mpasho wa RSS. Fuata hatua zilizo hapo chini ili uchapishe au uondoe mpasho wa RSS. Unaweza pia kupata maelezo zaidi kuhusu kupakia podikasti kutoka kwenye mipasho ya RSS katika YouTube.

Kumbuka: Kipengele cha Uingizaji wa RSS kinapatikana katika nchi au maeneo mahususi.

Jinsi ya Kupakia Podikasti za Sauti kwenye YouTube ukitumia Mipasho ya RSS

Kuunganisha mipasho ya RSS ili upakie podikasti kwenye YouTube

Kabla ya kuanza, ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube. Kisha, fuata hatua zilizo hapo chini ili upakie vipindi vya podikasti kutoka kwenye mipasho yako ya RSS kwenda YouTube.

Kuwasilisha mipasho ya RSS kwenye YouTube

1. Kwenye Studio ya YouTube, bofya Tayarisha  kisha Podikasti mpya kisha Wasilisha mipasho ya RSS .

Kumbuka: Ikiwa huna idhini ya kufikia vipengele vya kina, utahitaji kuthibisha utambulisho wako.

2. Soma na ukubali Sheria na Masharti ya Zana ya Uingizaji wa Data ya RSS. 

3. Soma maagizo kwenye skrini kisha ubofye Endelea.

4. Weka URL ya mipasho yako ya RSS kisha ubofye Endelea.

5. Bofya Tuma msimbo ili uthibitishe akaunti yako. 

6. Weka nambari ya kuthibitisha iliyotumwa kwenye anwani ya barua pepe iliyo kwenye mipasho yako ya RSS kisha ubofye Thibitisha. Ikiwa hujui barua pepe iliyo kwenye mipasho yako ya RSS, wasiliana na mtoa huduma wako wa upangishaji.

7. Chagua vipindi unavyotaka kupakia kwenye podikasti yako kwenye YouTube kisha ubofye Endelea. Unaweza kuchagua kupakia:

  • Vipindi vyote vilivyopo
  • Vipindi vilivyochapishwa tangu tarehe mahususi
  • Vipindi vya siku zijazo pekee
Ikiwa vipindi vyako vina matangazo yanayolipiwa, unapaswa pia kuteua chaguo la “Vipindi vingi kutoka kwenye mipasho ya RSS vina matangazo yanayolipiwa.” Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu bora za mipasho ya RSS kwenye YouTube.

8. Kagua maelezo ya uonekanaji kisha ubofye Hifadhi.

Kuchapisha podikasti kutoka kwenye mipasho yako ya RSS

Baada ya kuweka mipangilio ya mipasho yako, huenda siku kadhaa zikapita kabla ya vipindi vyako kupakiwa. Utapokea barua pepe podikasti yako inapokuwa tayari kuchapishwa. Hata hivyo, podikasti yako haitachapishwa hadi ufuate hatua zilizo hapo chini. 

Ili uchapishe mipasho,

  1. Kwenye Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Chini ya “Idadi ya video,” bofya Chapisha karibu na mipasho yako ya podikasti. Kitufe hiki kitaonekana tu ukishamaliza kupakia vipindi vya podikasti yako. 

Baada ya kuchapisha, podikasti yako na vipindi vyoyote vipya vitapatikana kwa umma ili kufikiwa na mtu yeyote kwenye YouTube. Unaweza kubadilisha mipangilio hii kwenye ukurasa wa Maelezo ya podikasti. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha uonekanaji chaguomsingi wa video kwenye sehemu inayofuata.

Kubadilisha maelezo ya podikasti

Ikiwa maelezo ya podikasti yaliyowasilishwa kwenye mipasho yako ya RSS hayapo au si sahihi, unaweza kuyabadilisha kwenye ukurasa wa Maelezo ya podikasti.

1. Kwenye Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
2. Wekelea kiashiria kwenye podikasti ambayo ungependa kuibadilisha kisha uchague Maelezo  Badilisha mpangilio, aikoni ya penseli.
3. Kwenye ukurasa wa maelezo ya Podikasti, sasisha mojawapo ya mipangilio ifuatayo:

  • Majina
  • Maelezo
  • Uonekanaji wa video
  • Mpangilio chaguomsingi wa video
  • Mipangilio ya RSS

4. Bofya Hifadhi ukikamilisha.

Kumbuka: Maelezo ya kipindi husasishwa kiotomatiki kwenye mipasho yako ya RSS. Ikiwa maelezo ya kipindi chako yatabadilika, unaweza kuyabadilisha ndani ya mipasho yako ya RSS. Ukibadilisha maelezo ya kipindi kwenye Studio ya YouTube, tutazuia mabadiliko yajayo ya kipindi hicho yanayofanywa ndani ya mipasho yako ya RSS.

Kuondoa mipasho ya RSS kwenye podikasti yako ya YouTube

Kuondoa mipasho yako ya RSS katika podikasti yako kwenye YouTube kutazuia vipindi vipya visipakiwe. 

  1. Kwenye Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Wekelea kiashiria kwenye podikasti ambayo ungependa kuibadilisha kisha uchague Maelezo  Badilisha mpangilio, aikoni ya penseli.
  3. Kwenye Ukurasa wa maelezo ya podikasti, tafuta kiungo cha mipasho yako ya RSS kisha ubofye Ondoa.
  4. Thibitisha kuwa ungependa kuondoa mipasho ya RSS kwenye kituo chako.

Kupakia upya kipindi

Ikiwa ungependa kusasisha faili ya sauti kupitia mipasho yako ya RSS, fuata hatua zilizo hapo chini ili upakie upya video yako.

  1. Kwenye Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Wekelea kiashiria kwenye podikasti ambayo ungependa kubadilisha kisha uchague Video .
  3. Wekelea kiashiria kwenye video ambayo ungependa kuingiza data upya kisha ubofye menyu .
  4. Chagua Pakia upya kutoka kwenye mipasho ya RSS

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14513138325163666230
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false