Kuzuia vituo katika hali ya matumizi yanayosimamiwa ya mtoto wako

Iwapo utaweka mipangilio ya matumizi yanayosimamiwa kwa ajili ya mtoto wako, unaweza kuzuia vituo mahususi kwa ajili yake kwenye YouTube. Ukibadilisha uamuzi wako kuhusu kituo ulichozuia, unaweza kukiruhusu kwenye YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.

Fuata hatua zilizo hapa chini za kuzuia na kuruhusu vituo.

Kuzuia chaneli za YouTube kwenye akaunti zinazodhibitiwa

Madokezo:
  • Anapotumia matumizi yanayosimamiwa, tayari mtoto wako anaona video chache kulingana na mipangilio ya maudhui ya akaunti yake. 
  • Iwapo mtoto wako anatumia Akaunti ile ile ya Google kwenye YouTube na YouTube Kids, vituo vyovyote vilivyozuiwa kwenye YouTube vitazuiwa pia kwenye YouTube Kids.
  • Hatua ya kuzuia kituo huzuia tu maudhui yaliyopakiwa kwenye kituo husika. Haizuii video zilizopakiwa upya kwenye vituo vingine au vituo kama hivyo vyenye maudhui yanayohusiana.

Zuia vituo husika kwenye YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa

Ili uzuie kituo mahususi kwenye YouTube katika kompyuta yako:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kituo cha YouTube unachotaka kuzuia.
  2. Nenda kwenye kichupo cha Kuhusu kwenye ukurasa wa kituo.
  3. Bofya Ripoti Mtumiaji .
  4. Chagua Zuia kituo kwa ajili ya watoto. Chaguo hili litaonekana tu iwapo unatumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.
  5. Dirisha ibukizi huenda likaonekana ili kukuarifu kuwa video kama hizo huenda bado zinapatikana kwenye vituo vingine. Bofya ENDELEA.
  6. Chagua ZUIA karibu na wasifu wa mtoto ambaye ungependa kuzuia asifuatilie kituo hiki.
  7. Kitufe cha ZUIA kitabadilika kuwa RUHUSU, kikikupatia chaguo la kutendua kitendo.
  8. Bofya NIMEKAMILISHA.

Ili uzuie kituo mahususi kwenye programu ya YouTube:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kituo cha YouTube unachotaka kuzuia.
  2. Gusa Zaidi ''.
  3. Gusa Zuia kituo kwa ajili ya watoto. Chaguo hili litaonekana tu iwapo unatumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.
  4. Dirisha ibukizi huenda likaonekana ili kukuarifu kuwa video kama hizo huenda bado zinapatikana kwenye vituo vingine. Gusa ENDELEA.
  5. Gusa ZUIA karibu na wasifu wa mtoto ambaye ungependa kuzuia asifuatilie kituo hiki.
  6. Kitufe cha ZUIA kitabadilika kuwa RUHUSU, kikikupatia chaguo la kutendua kitendo.
  7. Gusa Nimekamilisha .

Unaweza pia kuzuia maudhui moja kwa moja kwenye YouTube Kids katika kifaa cha mtoto wako.

Kuruhusu vituo mahususi kwenye YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa

Ili uruhusu vituo mahususi kwenye YouTube, ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa:

​Kwenye kompyuta:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kituo cha YouTube unachotaka kukiruhusu.
  2. Nenda kwenye kichupo cha Kuhusu kwenye ukurasa wa kituo.
  3. Bofya Ripoti mtumiaji .
  4. Chagua Zuia kituo kisitazamwe na watoto. Chaguo hili litaonekana tu iwapo unatumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.
  5. Dirisha ibukizi huenda likaonekana ili kukuarifu kuwa video kama hizo huenda bado zinapatikana kwenye vituo vingine. Bofya ENDELEA.
  6. Chagua RUHUSU karibu na wasifu wa mtoto ambaye ungependa kumruhusu afuatilie kituo hiki.
  7. Kitufe cha RUHUSU kitabadilika kuwa ZUIA, kikikupatia chaguo la kutendua kitendo.
  8. Bofya NIMEKAMILISHA.

Kwenye programu ya YouTube:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa kituo cha YouTube unachotaka kuruhusu.
  2. Gusa Zaidi ''.
  3. Gusa Zuia kituo kwa ajili ya watoto. Chaguo hili litaonekana tu iwapo unatumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.
  4. Dirisha ibukizi huenda likaonekana ili kukuarifu kuwa video kama hizo huenda bado zinapatikana kwenye vituo vingine. Gusa ENDELEA.
  5. Gusa RUHUSU karibu na wasifu wa mtoto ambaye ungependa kumruhusu afuatilie kituo hiki.
  6. Kitufe cha RUHUSU kitabadilika kuwa ZUIA, kikikupatia chaguo la kutendua kitendo.
  7. Gusa NIMEMALIZA.

Kuruhusu vituo vyote kwenye YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa

Ili uruhusu vituo vyote kwenye YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
    1. Iwapo unatumia kompyuta, chagua Dhibiti mipangilio ya mtoto wako, karibu na “Mipangilio ya Wazazi.”
  5. Chagua wasifu wa mtoto wako.
  6. Chini ya MIPANGILIO YA JUMLA, bofya Ruhusu video.
  7. Dirisha ibukizi huenda likaonekana ili kukuarifu kuwa maudhui yote uliyozuia kwenye YouTube na YouTube Kids yataruhusiwa. Chagua RUHUSU.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17609753144625617789
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false