Wazazi wanaoamua kuwa kijana wao mdogo (mtoto aliye na chini ya umri wa miaka 13 au umri unaofaa katika nchi au eneo waliko) yuko tayari kutazama maudhui kwenye YouTube wanaweza kufungua akaunti inayodhibitiwa. Kuna vidhibiti na mipangilio mbalimbali ya kukusaidia umwongoze kijana wako mdogo anapotazama maudhui kupitia matumizi yanayosimamiwa.
Kudhibiti mipangilio na vidhibiti vya wazazi
Unapomfungulia kijana wako mdogo Akaunti ya Google, unaweza kuweka vidhibiti vya wazazi ili atumie YouTube katika hali ya matumizi yanayosimamiwa kwenye Kituo cha Familia au Family Link.
Kutumia Kituo cha Familia cha akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa
- Ingia katika programu ya YouTube ukitumia akaunti yako ya mzazi iliyounganishwa.
- Gusa Wasifu kwenye kona ya chini kulia.
- Gusa Mipangilio .
- Chagua Kituo cha Familia.
Kutumia programu ya Family Link
Ili uangalie vidhibiti vya wazazi na mipangilio ya wasifu wa YouTube Kids au hali za utumiaji zinazosimamiwa kwenye YouTube katika Family Link:
- Kwenye kifaa chako, fungua programu ya Family Link .
- Chagua mtoto wako.
- Gusa Vidhibiti Vizuizi vya maudhui YouTube.
- Badilisha matumizi ya mtoto wako yanayosimamiwa kwenye mipangilio ya YouTube, chini ya "Mipangilio ya YouTube."
Kubadilisha mipangilio na vidhibiti mahususi vya wazazi
Unaweza kufanya matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube yamfae mtoto wako kwa kurekebisha mipangilio na vidhibiti mahususi vya wazazi. Vidhibiti na mipangilio hii hukuruhusu:
Kuzuia maudhui
Kubadilisha mipangilio ya kiwango cha maudhui
- Ingia katika YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
- Gusa Wasifu kwenye kona ya chini kulia.
- Chagua Mipangilio .
- Chagua Kituo cha Familia.
- Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
- Chagua BADILISHA karibu na “Mipangilio ya Maudhui.”
Family Link:
- Kwenye kifaa chako, fungua programu ya Family Link .
- Chagua mtoto wako.
- Gusa Vidhibiti Vizuizi vya maudhui YouTube.
- Badilisha mipangilio ya kiwango cha maudhui ya mtoto wako ili atumie YouTube katika hali ya matumizi yanayosimamiwa, katika “Mipangilio ya YouTube.”
Kukagua historia ya video alizotazama mtoto wako
Unaweza kukagua historia ya video ambazo mtoto wako ametazama katika akaunti yake inayodhibitiwa kwenye kifaa chake:
- Nenda kwenye ukurasa wa Shughuli Zangu.
- Chagua Historia ya YouTube.
- Chagua Dhibiti historia.
- Sogeza ili ukague historia ya video alizotazama.
Kufuta historia
Unaweza kufuta historia ya video zilizotazamwa na mambo yaliyotafutwa katika akaunti ya mtoto wako kwenye vifaa vyake vyote vilivyounganishwa kupitia YouTube:
- Ingia katika YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
- Gusa Wasifu kwenye kona ya chini kulia.
- Chagua Mipangilio .
- Chagua Kituo cha Familia.
- Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
- Bofya Futa historia.
- Ili uhifadhi mabadiliko uliyofanya, chagua FUTA.
Kuzima kipengele cha kucheza kiotomatiki
Unaweza kuzima kipengele cha Kucheza Kiotomatiki kwa niaba ya mtoto wako kwa kuchagua "Zima kipengele cha kucheza kiotomatiki". Mtoto wako hawezi kuwasha kipengele cha Kucheza Kiotomatiki wakati mipangilio hii imewekwa.
Ili umzimie mtoto wako kipengele cha kucheza kiotomatiki kwenye YouTube:
- Ingia katika YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
- Gusa Wasifu kwenye kona ya chini kulia.
- Chagua Mipangilio .
- Chagua Kituo cha Familia.
- Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
- Washa mipangilio ya Kuzima kipengele cha kucheza kiotomatiki.
Kusitisha historia ya video ulizotama
Unaweza kusimamisha video mpya zinazotazamwa zisitumiwe kama ishara za kupendekeza video nyingine.
Ili usitishe historia ya video alizotazama mtoto wako kwenye YouTube:
- Ingia katika YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
- Gusa Wasifu kwenye kona ya chini kulia.
- Chagua Mipangilio .
- Chagua Kituo cha Familia.
- Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
- Washa mipangilio ya Sitisha historia ya video alizotazama.
Kusitisha historia ya mambo aliyotafuta
Unaweza kusimamisha hoja mpya za utafutaji zisitumiwe kama ishara za kupendekeza video nyingine.
Ili usitishe historia ya mambo aliyotafuta mtoto wako kwenye YouTube:
- Ingia katika YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
- Gusa Wasifu kwenye kona ya chini kulia.
- Chagua Mipangilio .
- Chagua Kituo cha Familia.
- Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
- Washa mipangilio ya Sitisha historia ya mambo aliyotafuta.