Vidhibiti vya wazazi na mipangilio ya matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube

Wazazi wanaoamua kuwa mtoto wao aliye chini ya miaka 13 (au umri unaofaa katika nchi au eneo waliko) yuko tayari kutazama maudhui kwenye YouTube wanaweza kuweka mipangilio ya akaunti inayodhibitiwa. Kuna vidhibiti na mipangilio kadhaa kwa ajili yako ili kumwongoza mtoto wako anapotazama maudhui kupitia matumizi yanayosimamiwa.

Kumbuka: Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu vidhibiti vya wazazi na mipangilio ya YouTube Kids, pata maelezo zaidi kwenye Kituo chetu cha Usaidizi

Kudhibiti mipangilio na vidhibiti vya wazazi

Unapomfungulia mtoto wako Akaunti ya Google, unaweza kuweka vidhibiti vya wazazi kwa ajili ya matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube kupitia:

  • YouTube: Chini ya Vidhibiti vya Wazazi katika mipangilio ya YouTube ya akaunti ya mzazi iliyounganishwa
  • Family Link: Chini ya “Mipangilio ya YouTube” kwenye programu ya Family Link

Kutumia mipangilio yako ya YouTube ya akaunti ya mzazi iliyounganishwa

Ili uangalie mipangilio na vidhibiti vya wazazi kwa ajili ya matumizi yanayosimamiwa kwenye mipangilio yako ya YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
    1. Iwapo unatumia kompyuta, chagua Dhibiti mipangilio ya mtoto wako, karibu na “Vidhibiti vya Wazazi.”

Tumia programu ya Family Link

Ili uangalie vidhibiti vya wazazi na mipangilio ya wasifu wa YouTube Kids au hali za utumiaji zinazosimamiwa kwenye YouTube katika Family Link:

  1. Kwenye kifaa chako, fungua programu ya Family Link Family Link.
  2. Chagua mtoto wako.
  3. Gusa Vidhibiti kisha Vizuizi vya maudhui kisha YouTube.
  4. Badilisha matumizi ya mtoto wako yanayosimamiwa kwenye mipangilio ya YouTube, chini ya "Mipangilio ya YouTube."

Kubadilisha mipangilio na vidhibiti mahususi vya wazazi

Unaweza kufanya matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube yamfae mtoto wako kwa kurekebisha mipangilio na vidhibiti mahususi vya wazazi. Vidhibiti na mipangilio hii hukuruhusu:

Kuzuia maudhui

Unaweza kuingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa ili uzuie chaneli mahususi ambazo usingependa mtoto wako atazame.

Kubadilisha mipangilio ya kiwango cha maudhui ya mtoto wako 
Wazazi wanaweza kuchagua jinsi maudhui yatakavyochaguliwa katika matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube.

Kubadilisha mipangilio ya kiwango cha maudhui ya mtoto wako kwenye YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
  5. Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
  6. Iwapo ungependa kubadilisha mipangilio ya maudhui katika hali yake ya utumiaji inayosimamiwa kwenye YouTube:
    • Chini ya mipangilio ya YouTube, chagua BADILISHA karibu na “Mipangilio ya Maudhui.”

Iwapo unadhibiti Akaunti ya Google ya mtoto wako ukitumia Family Link, unaweza pia kubadilisha mipangilio yake ya kiwango cha maudhui kupitia programu ya Family Link:

  1. Kwenye kifaa chako, fungua programu ya Family Link Family Link.
  2. Chagua mtoto wako.
  3. Gusa Vidhibiti kisha Vizuizi vya maudhui kisha YouTube.
  4. Badilisha mipangilio ya kiwango cha maudhui ya mtoto wako katika matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube, chini ya “Mipangilio ya YouTube.”
Kumbuka: Utapata onyesho la kukagua maudhui yanayopatikana katika kila mipangilio ya maudhui ukibofya au kugusa jina la mipangilio ya maudhui. Unaweza kubadilisha mipangilio hii wakati wowote.
Kukagua historia ya video alizotazama mtoto wako

Unaweza kukagua historia ya video ambazo mtoto wako ametazama katika akaunti yake inayodhibitiwa kwenye kifaa chake:

  1. Nenda kwenye ukurasa wa Shughuli Zangu.
  2. Chagua Historia ya YouTube.
  3. Chagua Dhibiti historia.
  4. Nenda kwenye sehemu ya kagua historia ya video alizotazama.
Kufuta historia

Unaweza kufuta historia ya video zilizotazamwa na mambo yaliyotafutwa katika akaunti ya mtoto wako kwenye vifaa vyake vyote vilivyounganishwa kupitia YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
  5. Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
  6. Chagua Futa historia.
  7. Ili uhifadhi mabadiliko uliyofanya, chagua FUTA.
Kuzima kipengele cha kucheza kiotomatiki

Unaweza kuzima kipengele cha Kucheza Kiotomatiki kwa ajili ya mtoto wako kwa kuchagua "Zima kipengele cha kucheza kiotomatiki". Mtoto wako hawezi kuwasha kipengele cha Kucheza Kiotomatiki wakati mipangilio hii imewekwa.

Ili kuzima kipengele cha kucheza kiotomatiki kwa ajili ya mtoto wako kwenye YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
  5. Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
  6. Washa mipangilio ya Zima kucheza kiotomatiki.
Kusitisha historia ya video ulizotama
Unaweza kusimamisha video mpya zinazotazamwa zisitumiwe kama ishara za kupendekeza video nyingine.

Ili usitishe historia ya video alizotazama mtoto wako kwenye YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
  5. Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
  6. Washa mipangilio ya Sitisha historia ya video alizotazama.
Kusitisha historia ya mambo yaliyotafutwa
Unaweza kusimamisha hoja mpya za utafutaji zisitumiwe kama ishara za kupendekeza video nyingine. 

Ili usitishe historia ya mambo aliyotafuta mtoto wako kwenye YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya mzazi iliyounganishwa.
  2. Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
  3. Chagua Mipangilio .
  4. Chagua Vidhibiti vya Wazazi.
  5. Chagua akaunti au wasifu wa mtoto wako.
  6. Washa mipangilio ya Sitisha historia ya mambo yaliyotafutwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6575687570216545631
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false