Kuboresha video zako kwa kuweka manukuu

Baada ya kuhariri video zako, ziboreshe kwa kuweka manukuu. Fanya video ziweze kufikiwa na watazamaji wako kwa kutumia zana ya manukuu. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kunukuu au kuhariri kiotomatiki manukuu ya video yako.

Kumbuka: YouTube Create haiwezi kuzalisha manukuu kwenye klipu zenye urefu wa zaidi ya sekunde 60.
 
YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android ambazo zina angalau RAM ya 4GB. Huenda programu hii ikapatikana kwenye vifaa vingine katika siku zijazo.

Kuweka manukuu kwenye video zako

YouTube Create inaweza kuzalisha manukuu  kwa kugusa kitufe. Ili kuweka manukuu kwenye video,

  1. Fungua mradi kisha gusa Manukuu  kwenye upau wa vidhibiti.
  2. Kwenye Upau wa vidhibiti, chagua maudhui ambayo ungependa kunukuu:
  • Video zote huweka manukuu ya matamshi yoyote yaliyotambuliwa kwenye rekodi ya video halisi
  • Masimulizi huweka manukuu katika masimulizi yaliyorekodiwa kwenye programu tu
  1. Kwenye menyu ya "Lugha", chagua lugha iliyotumiwa kwenye masimulizi yako.
  2. Gusa Zalisha.

Hariri manukuu

Ikiwa manukuu si sahihi, tumia zana ya kuhariri ili kusasisha manukuu yanayoonyeshwa kwa watazamaji wako. Katika mradi unaoendelea kwenye zana ya kuhariri,

  1. Chagua safu ya manukuu yaliyozalishwa kwenye video yako.
  2. Gusa Badilisha 
  3. Katika manukuu, gusa neno lisilo sahihi.
  4. Andika ili usasishe maandishi.

Kubadilisha muundo wa manukuu

Unaweza kufanya manukuu yako yalingane na mandhari ya video yako kwa kubadilisha muundo wa maandishi ya manukuu. Katika mradi unaoendelea kwenye zana ya kuhariri,

  1. Chagua safu ya manukuu kwenye video yako.
  2. Gusa Muundo .
  3. Vinjari vichupo ili ubadilishe ukubwa, fonti, rangi, mandhari, muundo, muhtasari au kivuli.
  4. Gusa Nimemaliza ili uhifadhi mabadiliko.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14363873034895309258
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false