Kuweka maandishi kwenye video zako

Baada ya kutayarisha mradi, boresha video zako ukitumia zana za kuhariri video za YouTube Create. Wekea video zako mapendeleo ukitumia mamia ya fonti za Google zilizo katika lugha kadhaa.

YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android ambazo zina angalau RAM ya 4GB. Huenda programu hii ikapatikana kwenye vifaa vingine katika siku zijazo.

Kuweka maandishi kwenye video zako

  1. Katika mradi unaoendelea, gusa Maandishi  kwenye upau wa vidhibiti.
  2. Chagua Maandishi dhahiri  au Madoido ya maandishi .
  3. Andika ili uweke maandishi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka muundo wa maandishi hapa chini.
  4. Gusa Nimemaliza ukikamilisha.

Kubadilisha muundo wa maandishi

  1. Chagua safu ya maandishi ambayo ungependa kubadilisha kwenye mradi wako. 
  2. Kwenye upau wa vidhibiti, tumia chaguo zifuatazo ili ubadilishe maandishi:
    • Gawanya : Kata muda wa maandishi yako.
    • Badilisha : Andika ili ubadilishe maandishi yanayoonyeshwa kwenye video yako
    • Mtindo : Gusa kwenye vichupo ili ubadilishe ukubwa, fonti, rangi, mandhari, muundo, ukingo au kivuli.
    • Uhuishaji : Chagua uhuishaji na utumie vitelezi ili uweke muda wa madoido. 
  3. Gusa Nimemaliza ili usasishe maandishi.

Ili uhamishe safu ya maandishi kwenye video yako, iguse na uiburute hadi sehemu unapotaka kuiweka kwenye video yako.

Kufuta maandishi

  1. Gusa ili uchague safu ya maandishi unayotaka kufuta.
  2. Gusa Tupio .

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9055935525948036274
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false