Kuanzisha au kudhibiti mradi kwa kutumia YouTube Create

Ni rahisi kutayarisha video ndefu na Video Fupi kwa kutumia YouTube Create. Pakua programu na upate maelezo kuhusu jinsi ya kuanzisha mradi mpya.

NEW: YouTube Create App

YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android ambazo zina angalau RAM ya 4GB. Huenda programu hii ikapatikana kwenye vifaa vingine katika siku zijazo.

Kuanzisha mradi mpya

  1. Fungua programu ya YouTube Create na uingie katika akaunti yako ya YouTube.
  2. Kwenye skrini ya kwanza, gusa Ongeza  ili uanzishe mradi mpya.
  3. Katika matunzio, chagua picha, video au maudhui uliyopakia awali ili uyaweke kwenye mradi wako.
    • Kumbuka: Gusa Kishale cha kilicho karibu na Matunzio katika sehemu ya juu ya skrini ili upakie maudhui kutoka programu zingine kwenye kifaa chako. Unaweza kuweka picha au video nyingi kwenye mradi mmoja.
  4. Gusa Pakia ili uweke picha na video kwenye mradi wako.

Ukishaanzisha mradi wako, tumia zana za kuhariri ili uboreshe video yako.

Kutafuta, kudhibiti au kufuta mradi uliopo

  1. Fungua programu ya YouTube Create kisha uingie katika akaunti yako.
  2. Katika ukurasa wako wa Miradi ya Hivi Karibuni, gusa Menyu '' iliyo karibu na mradi ambao ungependa kudhibiti. Iwapo huoni mradi kwenye orodha, ingia kwa kutumia akaunti nyingine.
  3. Chagua kitendo kwenye chaguo:
    • Badilisha jina: Upe mradi wako jina jipya
    • Toa nakala: Toa nakala ya mradi wako
    • Futa: Futa mradi
  4. Thibitisha mabadiliko ukiombwa.
Unaweza pia kugusa Ongeza  katika orodha ya miradi ili utayarishe mradi mpya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10767416993094599359
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false