Kutatua hitilafu za upakiaji kwenye programu ya YouTube Create

Ikiwa unakumbwa na hitilafu kuhamisha au kupakia video yako iliyohaririwa kwenye YouTube Create, jaribu hatua hizi za utatuzi ili utatue hitilafu.

YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android ambazo zina angalau RAM ya 4GB. Huenda programu hii ikapatikana kwenye vifaa vingine katika siku zijazo.

Hitilafu za uhamishaji na upakiaji

Imeshindwa kuhamisha video iliyohaririwa kwenye programu ya YouTube Create

Vifaa vina uwezo tofauti wa kushughulikia miradi changamano. Huenda ukakumbwa na hitilafu za kuhamisha kwa sababu kifaa chako kimefikisha kiwango cha juu zaidi cha shughuli kinachoweza kutekeleza.

Jaribu kuondoa:

  • Safu za video, hasa zile zinazolingana (kwa mfano, popote kwenye mradi ambapo umeambatanisha safu nyingi)
  • Vibandiko
  • Madoido
  • Madoido

Kupunguza ubora wa kipengee unachohamisha:

  • Iwapo unahamisha kipengee chenye ubora wa 1080p, jaribu 720p

Tatizo la kushindwa kuhamisha huwa linajulikana na litaboreshwa kadiri muda unavyosonga.

Kuwasilisha maoni na picha za skrini:

  1. Katika kona ya juu kulia ya programu ya YouTube Create, gusa picha yako ya wasifu .
  2. Gusa Tuma maoni.

Matatizo ya kushindwa kupakia muziki au vibandiko

Muunganisho dhaifu wa mtandao unaweza kusababisha upakiaji wa vipengele kama vile muziki na vibandiko kuchukua muda mrefu. Jaribu kupakia vipengele hivyo tena muunganisho wako wa mtandao ukiwa thabiti.

Matatizo ya kuchapisha

Imeshindwa kupakia video kwenye YouTube kutoka YouTube Create

Kwanza, hakikisha kuwa mtandao wako ni thabiti.

Hakikisha kuwa umepakua programu ya YouTube. Ni lazima programu ya YouTube iwe imepakuliwa kwenye “wasifu” ule ule wa Android ambapo programu ya YouTube Create imepakuliwa. Vinginevyo, huwezi kukamilisha mchakato wa kuchapisha.

Hakikisha kuwa umeingia ukitumia akaunti ile ile kwenye programu ya YouTube Create na ya YouTube.

Ungependa kuchapisha video ya YouTube Create kwenye kituo tofauti

Video ya YouTube Create itahusishwa kiotomatiki na kituo kile kile ulichoingia kwenye programu ya YouTube Create. Ukishaanzisha mchakato wa kuchapisha, huwezi kubadilisha vituo.

Ili kurekebisha hali hii:

  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Gusa Tayarisha kisha Pakia video.
  3. Chagua video ya YouTube Create iliyohifadhiwa kwenye kifaa chako.

AU

  1. Ingia katika akaunti unayopendelea ambayo inahusishwa na kituo chako. Tayarisha mradi wako pale (miradi iliyo kwenye programu ya YouTube Create inahusishwa na akaunti yako).

Matatizo ya kufuta programu

Kupoteza video kutokana na kufuta programu

Kabla ya kufuta programu ya YouTube Create au kubadilisha ili utumie kifaa kipya, ni lazima uhamishie video zozote kwenye matunzio ya picha ya kifaa chako.

Iwapo utafuta programu kwenye kifaa chako au ukibadilisha na utumie simu mpya, miradi yoyote iliyopo itapotea.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6654246333618786347
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false