Kukagua, kupakia au kuhifadhi video kwa kutumia programu ya YouTube Create

Ukiwa tayari kuchapisha video yako, unaweza kupakia video yako moja kwa moja kwenye YouTube kutoka katika programu ya YouTube Create. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kukagua kwanza, kuhifadhi au kupakia mradi wako uliohaririwa ukitumia maelezo yaliyo hapa chini.

YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android ambazo zina angalau RAM ya 4GB. Huenda programu hii ikapatikana kwenye vifaa vingine katika siku zijazo.

Kukagua kwanza video ya YouTube Create

  1. Fungua programu ya YouTube Create na uingie katika akaunti yako ya YouTube.
  2. Kwenye ukurasa wa Miradi yako ya Hivi Karibuni, gusa kijipicha au jina la mradi ili ufungue mradi unaokusudia.
  3. Katika skrini ya kuhariri mradi, gusa Cheza ili ukague kwanza video.

Kuhifadhi video yako ya YouTube Create

  1. Katika mradi unaoendelea, gusa Zaidi  kwenye kona ya kulia.
  2. Gusa Hamisha .
  3. Gusa Kishale cha chini ili uchague ubora wa video unaopendelea.
  4. Gusa Hamisha ili uhifadhi mradi wako kwenye kifaa chako cha mkononi.

Kupakia video kutoka programu ya YouTube Create kwenye kituo chako

  1. Katika skrini ya kuhariri mradi uliotekelezwa kwenye programu ya YouTube Create, gusa Zaidi  kwenye kona ya kulia.
  2. Gusa Hamisha .
  3. Gusa Kishale cha chini ili uchague ubora wa video unaopendelea na uguse Hamisha .
  4. Gusa Pakia kwenye YouTube.
  5. Weka vitu kama vile jina, maelezo na kijipicha.
  6. Chagua kiwango cha faragha ya video yako. Unaweza pia kuchagua mahali au kuweka video kwenye orodha ya kucheza.
  7. Bofya Endelea ili uchague hadhira yako.
  8. Gusa Pakia video.
    • Kumbuka: Unaweza kupakia video ndefu na Video Fupi kutoka programu ya YouTube Create.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10197172567868187252
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false