Baada ya kutayarisha mradi, boresha video zako kwa kutumia zana za kuhariri za YouTube Create. Boresha vipengele vinavyoonekana katika video yako kwa kutumia urekebishaji wa rangi na madoido.
YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android (zilizo na angalau RAM ya GB 4) na iPhone XR pamoja na miundo mipya zaidi inayotumia iOS 17 au matoleo mapya zaidi katika nchi zote zilizoorodheshwa hapa. Programu hii inaweza kupatikana katika nchi au maeneo zaidi siku zijazo.
Kutumia madoido kwenye video zako
- Fungua mradi kisha uguse ili uchague klipu ya video ambayo ungependa kuhariri.
- Kwenye upau wa vidhibiti, gusa Madoido
.
- Vinjari na uchague madoido yaliyowekwa mapema kwenye chaguo. Unaweza kutumia kitelezi ili kubadilisha kiwango cha madoido.
- Gusa Nimemaliza ili utumie madoido kwenye video yako.
Kuweka madoido kwenye video zako
- Fungua mradi kisha uguse ili uchague klipu ya video ambayo ungependa kuhariri.
- Kwenye upau wa vidhibiti, gusa Madoido
.
- Vinjari na uchague madoido ya video kwenye chaguo.
- Gusa Nimemaliza ili utumie madoido kwenye video yako.
Kurekebisha rangi katika video zako
- Fungua mradi kisha uguse ili uchague klipu ya video ambayo ungependa kuhariri.
- Kwenye upau wa vidhibiti, gusa Rekebisha
.
- Tumia chaguo za usahihishaji wa rangi ili ubadilishe vipengele, kama vile utofautishaji wa video, ukolezaji na uwekaji rangi maalum. Unaweza kutumia kitelezi katika kila chaguo ili ubadilishe kiwango.
- Gusa Nimemaliza ili utekeleze marekebisho kwenye video yako.