Kuhariri Video Zako ukitumia Programu ya YouTube Create🎬🎞️🙌
YouTube Create ni programu inayokuwezesha uhariri video zako ukitumia zana muhimu za utayarishaji na zilizo rahisi kutumia. Tumia YouTube Create ili uhariri video ndefu na Video Fupi, bila kulipia wala kuonyeshwa matangazo.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupakua programu ya YouTube Create hapa chini au upate maelezo kuhusu jinsi ya kuanzisha mradi mpya.
Masharti ya kutumia YouTube Create
Ili upakue YouTube Create, ni lazima:
- Uwe na akaunti ya Google
- Uwe katika nchi au eneo ambapo YouTube Create inapatikana
- Tumia Android au iPhone (iPhone XR na miundo mipya zaidi inayotumia iOS 17 au matoleo mapya zaidi)