Kumbuka: Maudhui haya yanatumika tu na washirika wa muziki walio na makubaliano na YouTube kuhusu Video Fupi.
Muziki unaotimiza masharti ya kutumiwa kwenye Video Fupi zenye urefu wa dakika tatu
Kuanzia tarehe 15 Oktoba, 2024, video zote mpya za wima zenye urefu wa dakika 1 hadi 3 zitaainishwa kuwa Video Fupi kwenye YouTube. Kwa Chaneli Rasmi za Wasanii au chaneli zilizounganishwa na Mmiliki wa Maudhui ya muziki, tarehe ya mwisho ni tarehe 8 Desemba, 2025. Video Fupi zenye urefu unaozidi dakika moja zilizo na dai la hakimiliki linaloendelea, bila kujali sera, zitazuiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui yanayodaiwa yenye urefu unaozidi dakika moja katika Video Fupi za YouTube.
Dai likipatikana unapopakia Video fupi yenye urefu wa dakika 1 hadi 3, utapata arifa. Unaweza kuondoa maudhui yanayodaiwa kwenye video zako. Ikiwa unaamini kuwa dai lilifanywa kimakosa, unaweza kupinga dai. Baada ya dai kutatuliwa, Video yako fupi itaweza kutazamwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Video Fupi zenye urefu wa dakika moja hadi tatu.
Ili uepuke madai ya hakimiliki, unaweza kutumia muziki unaopatikana kwenye Maktaba ya Sauti ya Video Fupi. Kulingana na wimbo, unaweza kuweka hadi sekunde 90 za muziki kwenye Video yako fupi ya dakika 3 unapotumia zana za YouTube. Kuchagua sauti kutaonyesha sekunde za muziki zitakazochezwa. Unaweza pia kutumia muziki usio na mirabaha kutoka kwenye Maktaba ya Sauti ya YouTube. Muziki usio na mirabaha hautapokea dai la Content ID.
Video za Picha au Vipengee vya rekodi ya sauti
Ili wimbo uweze kutumika kwenye Video Fupi, kunapaswa kuwa na video ya picha na kipengee cha rekodi ya sauti kilichopachikwa ambavyo vimetimiza masharti yafuatayo:
- Video ya picha iwe inachezeka na iwe ilitolewa na mshirika aliye na makubaliano na YouTube kuhusu Video Fupi.
- Video ya picha haitapatikana katika maeneo ambako haichezeki.
- Kipengee cha video ya picha kiwe kimepachika kipengee cha rekodi ya sauti.
- Kipengee cha rekodi ya sauti kilichopachikwa kiwe kinamilikiwa na mshirika aliyekubali sheria na masharti ya Video Fupi za YouTube.
- Rekodi ya sauti haitapatikana kwenye Video Fupi katika maeneo ambako kipengee cha rekodi ya sauti hakina mmiliki au kinamilikiwa na mshirika ambaye hajakubali sheria na masharti ya Video Fupi.
- Kipengee cha rekodi ya sauti kiwe na sera ya zinazolingana ya video zinazochezeka na isiwe imewekwa kuwa 'zuia'.
- YouTube isiwe imetambua matatizo mengine yoyote ya idhini ya kutumia yanayohusiana na maudhui (k.m. uchapishaji).
Video za muziki
Ili video ya muziki itimize masharti ya kuandaa miseto kwenye Video Fupi, inapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:
- Video ya muziki ni ya umma.
- Video ya muziki iwe na dai moja kutoka kwenye kipengee cha video ya muziki
- Kipengee cha video ya muziki kiwe kinamilikiwa na mshirika ambaye amekubali sheria na masharti ya Video Fupi za YouTube.
- Ikiwa kuna maeneo ambako video ya muziki haimilikiwi au inamilikiwa na mshirika asiye na makubaliano ya Video Fupi, watumiaji hawataweza kuandaa mseto wakitumia video hiyo ya muziki katika maeneo hayo.
- Kipengee cha video ya muziki kiwe na sera ya zinazolingana ambayo haijawekwa kuwa 'zuia'.
- Kipengee cha Video ya Muziki hupachika kipengee cha rekodi ya sauti kinachomilikiwa na mshirika aliyekubali sheria na masharti ya YouTube kuhusu Video Fupi na ambaye ana sera ya zinazolingana ya video zinazochezeka. Ikiwa kipengee cha rekodi ya sauti hakina mmiliki katika eneo mahususi, video hiyo haiwezi kutumika katika Video Fupi katika eneo hilo.
- Ikiwa kipengee chako cha video ya muziki hakina kipengee cha rekodi ya sauti kilichopachikwa, unaweza kukiweka kwa kufuata hatua hizi.
- YouTube isiwe imetambua matatizo mengine yoyote ya idhini ya kutumia yanayohusiana na maudhui (k.m. uchapishaji).
Kumbuka: Ikiwa una shaka kuhusu upatikanaji wa maudhui yako kwenye Video Fupi, tafadhali wasiliana na timu ya usaidizi ya YouTube au msimamizi wako wa washirika, ikiwa yupo
Jinsi ya kuripoti matumizi mabaya
Sera na Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube unatumika kwenye miseto ya Video Fupi inayotumia maudhui ya video za muziki.
Ikiwa unaamini kuwa Video Fupi inayotumia maudhui yako ya video ya muziki inakiuka mwongozo na sera zetu zilizopo, unaweza kuiripoti kwa YouTube ukitumia hatua zilizoorodheshwa katika makala haya.