Unaweza kutiririsha mubashara sauti inayozingira ya 5.1 kwenye YouTube kwa watazamaji wanaotumia vifaa oanifu. Sauti inayozingira ya 5.1 hutumia spika zenye vipimo data kamili vitano, ikiwa ni pamoja na:
- Mbele kushoto
- Katikati
- Mbele kulia
- Sauti inayozingira kushoto
- Sauti inayozingira kulia
Pamoja na spika hizo tano, kuna spika ya madoido ya masafa ya chini iliyoundwa kwa ajili ya kipaza sauti cha sauti ya besi.
Ili utiririshe sauti inayozingira ya 5.1 kwenye YouTube Moja kwa Moja, ni lazima utayarishe maudhui ya sauti inayozingira ya 5.1 yanayooana na utumie programu ya kusimba inayooana.
Kumbuka kwamba unaweza tu kuingiza data ukitumia vifaa vya mono, stereo na sauti inayozingira ya 5.1. Mipangilio mingine ya spika ya sauti inaweza kusababisha ugeuzaji usiotegemewa kwenda stereo.
Weka mipangilio ya mtiririko wa sauti inayozingira ya 5.1 kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja
Unaweza kutumia itifaki za (uingizaji wa data) RTMP na HLS ili utume mitiririko yenye sauti ya 5.1. Ili mfumo utambue kiotomatiki vifaa vya kuingiza sauti inayozingira ya 5.1 na kuunda sauti inayozingira ya 5.1, ni lazima uunde funguo za mtiririko ukitumia mipangilio ya "Washa ubora unaoweka mwenyewe" iliyobatilishwa uteuzi kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
- Nenda kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja kwenye Studio ya YouTube, kisha bofya Unda Tiririsha Mubashara.
- Bofya menyu kunjuzi chini ya Ufunguo wa Mtiririko kisha uchague Unda Ufunguo mpya wa Mtiririko.
- Weka jina la ufunguo wa mtiririko, itifaki ya mtiririko na ubatilishe uteuzi wa kisanduku cha "Washa mipangilio unayoweka mwenyewe" chini ya ubora wa Mtiririko.
- Bofya Unda ili uhifadhi.
Mipangilio ya programu ya kusimba
Fuata mwongozo ili uone mipangilio ya jumla ya programu ya kusimba. Baadhi ya mipangilio mahususi ya sauti inayozingira ya 5.1 ni:
- Kodeki ya sauti: sauti inayozingira ya 5.1 inatumika tu katika AAC kwenye itifaki ya uingizaji (wa data) ya RTMP; kwa uingizaji (wa data) wa HLS, AAC, AC3 na EAC3 unatumika katika sauti inayozingira ya 5.1.
- Kasi ya sampuli ya sauti: KHz 48 kwa sauti inayozingira ya 5.1.
- Kasi ya biti ya sauti: Kbps 384 kwa sauti inayozingira ya 5.1.
Programu za kusimba zinazooana
Zifuatazo ni programu za kusimba zinazojulikana za kutiririsha sauti inayozingira ya 5.1 kwenye YouTube Moja kwa Moja. Programu nyingi zaidi za kusimba zitaongezwa kadiri zinavyojaribiwa.
Programu za kusimba
Programu za kusimba za maunzi