Kutafuta podikasti kwenye YouTube Music

Ukiwa na YouTube Music, unaweza kusikiliza podikasti unazopenda. Pata maelezo ya jinsi ya kuvinjari na kutafuta podikasti kwenye programu ya YouTube Music.

Kumbuka: Watumiaji walio katika nchi au maeneo mahususi huenda wakakumbana na hali tofauti ya utumiaji wa bidhaa.

Gundua podikasti kwenye kichupo cha Ukurasa wa Mwanzo

Pata mapendekezo mapya ya podikasti na vipindi visivyokamilika kwenye kichupo cha Ukurasa wa Mwanzo . Ili uchuje mapendekezo yako, gusa Podikasti katika sehemu ya juu ya Skrini yako ya kwanza.

Gundua podikasti mpya

Kichupo cha Gundua  hukuwezesha upate podikasti mpya ili uongeze maudhui kwenye maktaba yako. Angalia podikasti na vipindi maarufu katika nchi au eneo lako au vinjari kulingana na aina, ikiwa ni pamoja na:

  • Biashara
  • Vichekesho
  • Michezo ya Video
  • Afya na Siha
  • Muziki
  • Jamii na Utamaduni
  • Uhalifu Halisi

Tafuta podikasti

Unaweza pia kutafuta vipindi vinavyopatikana. Chuja Podikasti au Vipindi katika sehemu ya juu ya ukurasa wa utafutaji ili upunguze orodha ya matokeo yako.

Vinjari ukurasa wa kituo

Ukurasa wa kituo huonyesha podikasti na vipindi vingine kutoka kwa mtayarishi mahususi. Unaweza pia kuvinjari ili uonyeshe maelezo, uweke podikasti kwenye mkataba yako au upakue vipindi kwenye ukurasa wa kituo.

Ili uende kwenye ukurasa wa kituo, bofya jina la kituo kwenye kipindi cha podikasti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11811409453365090752
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false