Pata na utumie Ofa zako za Premium

Ukiwa mwanachama wa YouTube Premium, unaweza ukastahiki kutumia ofa maalum za bidhaa na uanachama mahususi. Matoleo mapya yanatangazwa kwenye makala yetu ya Masasisho ya Premium, hivyo angalia mara kwa mara ili upate taarifa mpya!

Masharti ya ofa

  • Baadhi ya ofa hazipatikani kwenye nchi/maeneo yote.
  • Mipango ya wanafunzi haitii masharti ya Ofa za Premium.
  • Baadhi ya ofa zinaweza kupatikana tu ili zitumike kutoka kwenye kompyuta au kivinjari. Ikiwa unatatizika kutumia ofa kutoka kwenye programu ya YouTube, jaribu tena kupitia youtube.com.
  • Ikiwa huwezi kutumia ofa, angalia kama umeingia kwenye akaunti yako ya YouTube Premium. Iwapo bado unatatizika, wasiliana na timu ya usaidizi.

Pata ofa mpya

Fuata hatua zilizo hapa chini ili uvinjari Ofa za Premium zinazopatikana.
  1. Fungua youtube.com na uingie katika akaunti yako ya YouTube Premium.
  2. Vinjari Ofa Zako kwenye ukurasa wa kwanzaili upate maelezo zaidi kuhusu vipindi vya kujaribu na matoleo yanayopatikana.

Tumia ofa

  1. Fungua ofa unayotaka kutumia.
  2. Nakili Msimbo wa Ofa kutoka kwenye ukurasa wa maelezo ya ofa.
  3. Bofya Tumia. Utaelekezwa kwenye ukurasa wa mbele ya duka linalotoa ofa.
  4. Wakati wa kulipa, weka msimbo wa ofa ulionakili kutoka kwenye ukurasa wa Ofa za Premium.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11695910268369492320
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false