Kutumia kipengele cha SharePlay kutazama video za YouTube na watu wengine

Unaweza kutumia SharePlay kutazama video za YouTube pamoja na watu wengine huku ukipiga simu ya FaceTime. Kwanza, mwanachama wa YouTube Premium atahitaji kuanzisha kipindi cha kushiriki moja kwa moja. Kipindi cha kushiriki kikishaanza, watu wengine wanaweza kujiunga kwenye simu hiyo bila kuwa na uanachama wa Premium.

Kumbuka:

  • Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana kwenye vifaa vya iPhone na iPad pekee.
  • Ni lazima uwe umeingia kwenye YouTube ukitumia Akaunti yako binafsi ya Google.

SharePlay

Ili uanze kushiriki kipindi:

  1. Mwanachama wa YouTube Premium: Kwanza, ingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Kisha, anzisha simu ya FaceTime.
  3. Ukiwa kwenye simu ya FaceTime, gusa kitufe cha Kushiriki Maudhui kisha uchague YouTube. Unaweza pia kufungua programu ya YouTube wakati simu yako ya FaceTime inaendelea.
  4. Cheza video unayotaka mtazame pamoja. Utaombwa uthibitishe kuwa unataka kutazama video hiyo pamoja na kila mtu kwenye simu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14838082436521369069
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false