Matangazo kwenye video zilizopachikwa

Tumerahisisha chaguo za miundo ya matangazo yanayoonyeshwa kabla au baada ya video yako kucheza ili kuongeza mapato ya mtayarishi. Tumeondoa chaguo za matangazo mahususi kwa matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika. Sasa unapowasha matangazo kwenye video ndefu mpya, tunawaonyesha watazamaji wako matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika panapofaa. Badiliko hili linafanya mbinu bora zinazopendekezwa za kuwasha miundo yote ya matangazo zifae kwa kila mtu. Chaguo zako za matangazo yanayochezwa katikati ya video hazijabadilika. Pia, tumehifadhi chaguo zako za matangazo katika video ndefu zilizopo, isipokuwa ukibadilisha mipangilio ya uchumaji wa mapato.

Huenda video zilizopachikwa zikaonyesha matangazo yanayorukika au yasiyorukika video inapocheza. Tovuti yoyote au programu ya vifaa vya mkononi ambayo inapachika video, ikijumuisha tovuti au programu yako binafsi, inaweza kukuzalishia mapato. Pata maelezo zaidi kuhusu Miundo ya matangazo ya YouTube.

Kuwasha au kuzima matangazo kwenye video zilizopachikwa

Unapowasha matangazo kwenye kituo chako, unaweza kushiriki mapato yanayotokana na matangazo yanayoonyeshwa ndani ya Kicheza Video cha YouTube kilichopachikwa kwenye programu au tovuti nyingine. Kumbuka kuwa video zilizopachikwa zitatumia mipangilio sawa ya kuwezesha matangazo kama inayotumika kwenye video katika youtube.com.

Ikiwa umeunganisha akaunti zako za YouTube na AdSense katika YouTube na umeruhusu upachikaji wa video, utakuwa umechagua kiotomatiki kuonyesha matangazo. Kumbuka kuwa video zilizopachikwa zitatumia mipangilio sawa ya kuwezesha matangazo kama inayotumika kwenye video katika youtube.com.

Ikiwa hutaki kuonyesha matangazo kwenye video zako zilizopachikwa, hakuna njia ya kuzima matangazo moja kwa moja kwenye video zilizopachikwa pekee. Unaweza kuzima upachikaji.

Masharti ya matangazo kwenye video zilizopachikwa

Matangazo huonekana kwenye tovuti zinazofaa chapa: YouTube hufanya kazi kwa bidii ili chapa za watangazaji wetu zionekane kwenye tovuti zinazoendana na maadili yetu ya msingi. Mifumo yetu hutathmini kwa karibu tovuti na maudhui kwa vigezo mbalimbali ili kubaini iwapo iwashe matangazo wakati wa utiririshaji kwenye vipachikwa vya YouTube. Vigezo hivi vinajumuisha mwongozo madhubuti kuhusu maudhui kama vile picha za watu wazima, vurugu, lugha ya chuki na isiyofaa na tovuti zinazohamasisha ukiukaji.

Maelezo ya kichezeshaji: Tunahitaji kicheza video kionekane kwa ukubwa wa kutosha ili kukuza hali bora ya utumiaji. Tunapendekeza kichezaji cha pikseli 200 kwa 200 au kubwa ya hiyo. Pia, video zinapaswa kupachikwa kwa kutumia upachikaji wa kawaida wa kubofya ili kucheza na si uchezaji uliowekwa kwa misimbo.

Ugavi wa mapato kwenye video zilizopachikwa

YouTube na mmiliki wa video pekee ndio wanaweza kuchuma mapato kutokana na matangazo katika video zilizopachikwa. Mmiliki wa tovuti ambako video imepachikwa hatapata mgawo wa mapato.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5738858682470483343
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false