Pata maelezo kuhusu maoni yasiyoonekana au yaliyoondolewa

Maoni ni sehemu muhimu ya kukuza jumuiya kwenye YouTube. Lakini huenda maoni yako yasionekane au yakaondolewa. Soma makala haya ili upate maelezo kuhusu baadhi ya sababu.

Maoni yangu hayaonekani

Ikiwa huoni maoni yako kwenye sehemu ya maoni Maarufu, panga maoni kulingana na "Mapya zaidi kwanza".

  1. Nenda kwenye maoni.
  2. Bofya Panga kulingana na kisha Mapya zaidi kwanza.
  3. Nenda kwenye maoni yako. Ikiwa maoni yako hayataonekana kwenye mwonekano wa Mapya zaidi kwanza, huenda yalidhibitiwa na chaneli au kuondolewa kwa ukiukaji wa sera.

Kuhusu maoni Maarufu na maoni ya Wanachama

Mwonekano wa maoni Maarufu huonyesha maudhui ambayo watazamaji wanaweza kuyathamini au kutagusana nayo kulingana na ishara mbalimbali, kama vile maandishi ya maoni, maandishi ya kitambulishi, maandishi ya jina la kituo, ishara na video.

Mwonekano wa maoni huonyesha maoni ya wanachama wa kituo, yaliyopangwa kulingana na maoni mapya zaidi kwanza.

Kumbuka: Mwonekano wa maoni ya wanachama huonekana kwenye vifaa vya mkononi vya Android pekee.

Huenda mwonekano wa maoni Maarufu na maoni ya Wanachama usionyeshe maudhui ambayo YouTube imeyatambua kuwa huenda watazamaji wasiyathamini au kutagusana nayo. Hii inaweza kujumuisha maoni ambayo yametambuliwa kuwa huenda hayafai, taka au yanaiga mtu mwingine, kulingana na ishara mbalimbali, kama vile maandishi ya maoni, maandishi ya jina la kituo cha anayetoa maoni au maandishi ya kitambulishi, ishara na mipangilio ya udhibiti wa kituo. Ukiwa kwenye mwonekano wa maoni Maarufu, maoni maarufu ya wanachama wa kituo yanaweza kuonekana katika sehemu maalum inayoitwa 'Maoni kutoka kwa wanachama'.

Pata maelezo kuhusu udhibiti na uondoaji wa maoni

Hizi ni sababu chache zinazofanya huenda maoni yako yasionekane:

  • Uondoaji wa kiotomatiki: Mifumo yetu ya utambuzi wa kiotomatiki huchanganua maoni mara kwa mara ili kubaini iwapo yanakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya. Mfumo wetu ukitambua kuwa maoni yako yanakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, basi maoni hayo yataondolewa.
Kumbuka: Kuchapisha maoni mengi kwa muda mfupi, kuchapisha maoni sawa mara kwa mara, kushiriki viungo au matumizi yaliyokithiri ya emoji au herufi zisizo za kawaida yanaweza kutambuliwa kuwa taka na kuondolewa kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube.
  • Ripoti: Ikiwa mtu ataripoti maoni yako na iwapo yatakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, yataondolewa.
  • Udhibiti wa kituo:
    • Kituo kinaweza kuzuia maoni yote au ambayo yanaweza kuwa hayafai ili yakaguliwe. Kituo kinapozuia maoni ili yakaguliwe, mmiliki wa kituo au mdhibiti anatakiwa kuidhinisha maoni kabla hayajachapishwa. Kama mipangilio chaguomsingi, maoni yanayoweza kuwa hayafai yanazuiwa kiotomatiki katika vituo ili yakaguliwe.
    • Mmiliki wa Kituo anaweza kuchagua maneno na vifungu vya maneno ambavyo hahitaji vionekane kwenye sehemu ya maoni katika vituo vyao. Ikiwa maoni yako yana neno au kifungu cha maneno kilichozuiwa, hayataonekana.
    • Kituo kinaweza kuondoa maoni yako.

Iwapo wewe ni mmiliki wa kituo na maoni yameondolewa kwenye video zako, inawezekana kabisa kuwa YouTube imetambua vitndo vya ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya kwenye maoni.

Makala yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13361900760819888577
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false