Rekebisha hitilafu za kujisajili kwenye YouTube Premium na YouTube Music Premium

Ukipokea ujumbe wa hitilafu unapojaribu kujiunga na YouTube Premium au YouTube Music Premium, tafuta ujumbe husika wa hitilafu hapa chini ili utatue na urekebishe tatizo.

"Hatukuweza kuthibitisha nchi yako"

YouTube inahitaji kuthibitisha nchi yako ili ikuonyeshe mipango na ofa zinazopatikana kwa ajili yako. Ukipokea ujumbe unaosema, "Hatukuweza kuthibitisha nchi yako," fuata hatua zilizo hapa chini ili utatue tatizo hilo.

  • Unganisha kwenye mtandao tofauti.
  • Tumia kifaa tofauti.
  • Kununua YouTube Premium kwenye programu ya vifaa vya mkononi:
  1. Fungua programu ya YouTube kwenye kompyuta kibao au simu yako.
  2. Ingia katika akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kwa ajili ya kuanzisha uanachama wako.
  3. Chagua picha ya wasifu wako  > Jisajili kwenye YouTube Premium au Jisajili kwenye Music Premium.
  4. Ikiwa unastahiki, anza kipindi chako cha kujaribu. Vinginevyo, fuata hatua ili uanzishe uanachama wako unaolipiwa.
Iwapo unatumia VPN au huduma ya seva mbadala, tafadhali rejelea kituo cha usaidizi cha huduma au tovuti ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuizima. Baada ya kumaliza, jisajili kwenye uanachama wako katika youtube.com/premium au youtube.com/musicpremium.

Akaunti za Workspace

  • Huwezi kujisajili kupata uanachama binafsi au wa familia kwenye YouTube Premium ukitumia akaunti ya Workspace, isipokuwa kama ni akaunti ya toleo binafsi la Workspace.
  • Unaweza kujisajili ili upate mpango wa wanafunzi wa YouTube Premium ukitumia akaunti yoyote ya Workspace.
  • Iwapo unafikiri kuwa unastahiki kipindi cha kujaribu lakini huoni chaguo lake, badilisha utumie akaunti yako binafsi na ujisajili katika youtube.com/premium.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17310760581907278783
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false