Kutimiza masharti ya kutumia mfumo wa Content ID

Kuna vigezo kadhaa vinavyofanya mtu awe ametimiza masharti ya kutumia mfumo wa Content ID . Vigezo hivi ni pamoja na iwapo maudhui ya mwenye hakimiliki yanaweza kudaiwa kupitia mfumo wa Content ID na iwapo ameonyesha kuwa kuna hitaji. Ni sharti wenye hakimiliki watoe ushahidi wa maudhui yaliyo na hakimiliki ambayo ni wao tu walio na haki za kuyadhibiti.

Mfumo wa Content ID utaangalia maudhui yako ya marejeleo na kuyalinganisha na kila maudhui yaliyopakiwa kwenye YouTube. Ni sharti wenye hakimiliki wawe na haki za kipekee kwa maudhui yanayofanyiwa tathmini. Mifano ya kawaida ya vipengee ambavyo huenda visiwe vya kipekee kwa watu binafsi ni pamoja na:

  • ​programu ya kuchanganya, orodha ya miziki, mikusanyiko na miseto ya kazi nyingine
  • uchezaji wa video, programu za kutazama video, vionjo
  • muziki na video ambayo haina leseni
  • muziki au video iliyopewa leseni lakini si kwa kipekee
  • rekodi za maonyesho ya moja kwa moja (ikiwa ni pamoja na tamasha, matukio, hotuba, maonyesho)

Ikiwa mwenye hakimiliki ameidhinishwa kutumia mfumo wa Content ID, ni sharti ajaze mkataba. Mkataba huu utasema moja kwa moja kwamba ni maudhui yenye haki za kipekee tu ndizo zinaweza kutumiwa kwa marejeleo. Pia, atahitaji kutoa maelezo ya mahali kijiografia ya umiliki wa kipekee, kama si wa kote duniani.

Kando na Content ID, tuna zana nyingine za udhibiti wa hakimiliki ambazo huenda zikakidhi mahitaji ya mwenye hakimiliki.

Zana hizi zingine ni pamoja na:

  • Fomu ya wavuti ya kutuma malalamiko kuhusu hakimiliki
  • Mpango wa Kuthibitisha Maudhui (CVP)
  • Copyright Match Tool

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu chaguo hizi hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2364274657249571540
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false