Ulengaji wa umri na matangazo

Vizuizi vya Umri kwenye YouTube:

Video au chaneli maalum huwekewa kizuizi cha umri na chaguo la mtangazaji au baada ya ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya. Watazamaji “waliotimiza umri” ndio tu wanaoweza kutazama maudhui haya wakiwa wameingia katika akaunti kwenye YouTube. Wakati mwingine, ni lazima video iwekewe kizuizi cha umri kabla mtangazaji hajaitumia kwenye tangazo (kama vile tangazo la Video kwenye kampeni ya pombe). Kizuizi cha Umri kwenye YouTube ndicho chaguo la pekee linalopatikana kwa maombi ya kuweka vizuizi vya umri kwenye ukurasa wa kutazama video.

Ulengaji wa demografia kulingana na umri kwa ajili ya matangazo:

Sera zetu au watangazaji wakati mwingine huomba tangazo lilenge defografia fulani ya umri. Teknolojia yetu ya kuonyesha matangazo inaweza kulenga matangazo haya kulingana na tarehe za kuzaliwa za watumiaji wa YouTube walioingia katika akaunti. Kwa mfano, ikiwa tangazo halifai hadhira ya jumla kwa mujibu wa sera zetu, ni lazima tangazo hilo lilenge watazamaji walio na umri wa miaka 18 na zaidi. Hii inamaanisha kuwa watazamaji walioingia katika akaunti ambao wana angalau umri wa miaka 18 ndio tu watakaopata tangazo hili kwenye tovuti yetu. Watazamaji walioondoka kwenye akaunti watapata tangazo tofauti.

Vizuizi Maalum vya Umri:

Watangazaji wa pombe, michezo ya video na filamu wanaweza kubuni vizuizi maalum vya umri kwenye matangazo ya ukurasa wa kwanza. Tunaruhusu hali hii kwa sababu hizi ni sekta zenye udhibiti mkubwa na huenda kizuizi cha umri cha YouTube kisitimize kanuni za sekta. Kwa mfano, huenda watangazaji wa michezo ya video wakahitaji kufuata mwongozo wa ESRB kwenye mchezo wenye ukadiriaji wa ukomavu. Maombi ya kizuizi maalum cha umri kutoka kwa watangazaji hawa yanahitaji kutumwa kwa timu ya YouTube ya Sera za Matangazo ili yaidhinishwe kwanza. Watangazaji kwenye sekta nyingine zote ni sharti watumie vipengele vya kawaida vya Kizuizi cha Umri cha YouTube vinavyopatikana kwenye chaneli maalum na kurasa za kutazama video.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14867503288259925538
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false