Mabadiliko ya sheria na masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube

Hivi majuzi tulitangaza jinsi tunavyopanua na kubadilisha Mpango wa Washirika wa YouTube (YYP) kwa kuzindua masharti mapya ya kutayarisha Video Fupi, njia mpya za kuchuma mapato kwenye YouTube (ikiwa ni pamoja na ugavi wa mapato ya matangazo kwenye Video Fupi) na kutoa idhini ya kufikia Muziki wa Watayarishi.

Ili kuwezesha mabadiliko haya, tunaongeza sheria na masharti mapya ya Mpango wa Washirika wa YouTube. Endelea kusoma ili uelewe mabadiliko ya hivi karibuni ya sheria na masharti haya kisha uchukue hatua ili uhakikishe kuwa chaneli yako inaendelea kuchuma mapato.

Tunakuletea Sehemu

Tumerekebisha sheria na masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube ili kujumuisha Sehemu mpya zinazowapatia watayarishi urahisi zaidi katika njia wanazoweza kuchuma mapato kupitia maudhui yao. Baada ya kukubali Sheria na Masharti ya Msingi, ambayo ni masharti muhimu kwa watayarishi wote wanaotamani kuchuma mapato katika mfumo, watayarishi wanaweza kuchagua kwenye Sehemu za masharti ili kufungua fursa za kuchuma mapato.

Masharti ya Msingi

Masharti ya Msingi yanajumuisha sheria na masharti muhimu ya mpango kama vile jinsi tunavyokulipa, sera zetu za maudhui na sheria na masharti mapya kama vile gharama za kuonyesha maudhui katika nchi na marekebisho ya kuidhinisha haki. Watayarishi wote walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube au wanaotarajia kujiunga wanahitajika kukubali Masharti ya Msingi.

Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama

Ukurasa wa Kutazama huwakilisha kurasa zilizo kwenye YouTube, YouTube Music na YouTube Kids zinazojikita katika maelezo na uchezaji wa video zako ndefu au zinazotiririshwa mubashara. Ili uchume mapato ya matangazo na YouTube Premium kwenye video ndefu au zinazotiririshwa mubashara, zilizotazamwa kwenye Ukurasa wa Kutazama au zinapopachikwa kwenye tovuti nyingine katika Kicheza Video cha YouTube, utahitaji kukubali Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama. Kwa watayarishi waliopo katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP), hii inamaanisha kuwa utahitajika kukubali sehemu hii ili uendelee kuchuma mapato ya matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama.

Sehemu ya Uchumaji Mapato katika Video Fupi

Sehemu ya Uchumaji Mapato katika Video Fupi huruhusu chaneli yako kugawana mapato yanayotokana na matangazo yaliyotazamwa katikati ya video katika Mipasho ya Video Fupi. Ukishakubali Sehemu hii, utaanza kuchuma mapato kutokana na matangazo ya Mipasho ya Video Fupi na mapato ya YouTube Premium kwenye idadi inayotimiza masharti ya mara ambazo Video zako Fupi zilitazamwa kuanzia tarehe 1 Februari, 2023. Iwapo utakubali baada ya tarehe 1 Februari, 2023, ugavi wa mapato ya matangazo ya Video Fupi utaanza kutekelezwa kuanzia tarehe uliyokubali. Ili upate maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa ugavi wa mapato ya matangazo kwenye Video Fupi, soma Sera zetu za uchumaji wa mapato katika Video Fupi za YouTube.

Sehemu ya Bidhaa za Biashara

Sehemu ya Bidhaa za Biashara (awali ilijulikana kama Masharti ya Ziada ya Bidhaa za Biashara) hufungua mkusanyiko wa vipengele vya Ufadhili Kutoka kwa Mashabiki, vikijumuisha uanachama katika chaneli, Super Chat, Super Stickers na Shukrani Moto, vinavyokusaidia kuchuma mapato huku ukiwasiliana na mashabiki zako. Sheria na Masharti haya hayabadiliki, kwa hivyo ikiwa tayari umeyakubali, hutahitaji kuyakubali tena.

Nini kitatokea ikiwa hutakubali sheria na masharti mapya

Ni muhimu kwa washirika wote kusoma na kuelewa sheria na masharti mapya ya Mpango wa Washirika wa YouTube. Ili ujiunge au uendelee kuwepo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unahitaji kukubali Masharti ya Msingi.

Ugavi wa mapato ya matangazo kwenye Video Fupi utaanza tarehe 1 Februari, 2023. Ili kuanza kuchuma mapato ya matangazo kulingana na idadi ya mara ambazo Video Fupi zilitazamwa, washirika wanaochuma mapato watahitaji kukubali Sheria na Masharti ya Msingi na Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Video Fupi. Hutaweza kuchuma mapato kutokana na matangazo ya Mipasho ya Video Fupi mpaka ufanye hivyo. Idadi ya mara ambazo Video Fupi zilitazamwa iliyopatikana kabla ya kukubali Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Video Fupi haizingatiwi katika ugavi wa mapato ya matangazo kwenye Video Fupi.

Ili kubaki katika Mpango wa Washirika wa YouTube na kuendelea kuchuma mapato kwenye YouTube, washirika wote wanaochuma mapato wanahitajika kusoma na kukubali sheria na masharti mapya kufikia 10 Julai, 2023. Iwapo hutakubali angalau Masharti ya Msingi kufikia tarehe hiyo, chaneli yako itaondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube na makubaliano yako ya uchumaji wa mapato yatasimamishwa. Baada ya hayo kutokea, utahitaji kutimiza tena masharti na kutuma upya maombi ili ujiunge tena.

Baada ya chaneli yako kuondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP), kumbuka kuwa Sheria na Masharti ya YouTube bado yanatumika na yanasimamia matumizi yako ya YouTube. Hii inajumuisha haki ya YouTube kuchuma mapato na kuonyesha matangazo kwenye maudhui yako. Ikiwa kwa sasa hujajiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, lakini ulikuwepo awali, bado unaweza kuendelea kuona matangazo yanayoonyeshwa kwenye maudhui yako, lakini hutakuwa na haki ya kupata malipo.

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini mmeamua kutenga sheria na masharti katika sehemu mahususi?

Hatua ya kuzindua Sehemu kwenye Sheria na Masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube inamaanisha kuwa tunaweza kuweka fursa mpya za uchumaji wa mapato katika siku zijazo bila kusasisha au kurekebisha makubaliano yote ya uchumaji wa mapato.

Pia, mbinu hii huwapa watayarishi uwazi na umakini mkubwa wa kuamua ni fursa zipi za uchumaji wa mapato zinafaa chaneli zao.

Je, ninaweza kujiondoa kwenye baadhi ya Sehemu baada ya kuzikubali?

Ndiyo. Unaweza kujiondoa kwenye baadhi ya Sehemu mahususi za uchumaji wa mapato wakati wowote kwa kuwasiliana na Usaidizi kwa Watayarishi.

Je, hali hii inafanyaje kazi kwenye chaneli zilizo kwenye Mtandao wa Chaneli Mbalimbali (MCN)?

Washirika wote wanaochuma mapato wanahitajika kukubali Sheria na Masharti mapya ya Msingi kufikia tarehe 10 Julai, 2023 ili waendelee kuchuma mapato. Iwapo msimamizi wa Mtandao wa Chaneli Mbalimbali hatakubali sheria na masharti kufikia tarehe 10 Julai, lakini chaneli ya mshirika wake ikakubali, basi chaneli ya mshirika itaondolewa kwenye Mtandao wao wa Chaneli Mbalimbali na kuchukuliwa sawa na washirika wengine katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) bila kuathiri hali ya chaneli hiyo ya uchumaji wa mapato.

Ninapaswa kujua nini ikiwa ninatumia Kidhibiti Maudhui cha Studio (CMS)?

Washirika wanaoweza kutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio (CMS) watahitajika kukubali Marekebisho ya Masharti ya Uchumaji wa Mapato yanayojumuisha uchumaji wa mapato kwenye maudhui ya video zako ndefu katika Ukurasa wa Kutazama. Pia, yanajumuisha masharti muhimu ya mpango kama vile jinsi tunavyokulipa, sera zetu za maudhui na masharti mapya kama vile gharama za kuonyesha maudhui katika nchi, marekebisho ya kuidhinisha haki na maudhui yanayofaa kutumika katika kuandaa mseto. Washirika ambao wangependa kutumia ugavi wa mapato ya matangazo kwenye Video Fupi pia watahitaji kukubali Sehemu ya Uchumaji wa Mapato katika Video Fupi.

Partners using YouTube Studio Content Manager will also need to review and accept new terms by July 10, 2023. Iwapo hutakubali angalau Marekebisho ya Masharti ya Uchumaji wa Mapato kufikia tarehe hiyo, makubaliano yako ya uchumaji wa mapato yatasimamishwa na chaneli zako hazitaweza kuchuma mapato kwenye YouTube.
Je, masharti mapya ya “Mapato Yasiyotimiza Vigezo” yana maana gani kwa uchumaji wa mapato?

Masharti ya YouTube yanasaidia kuhakikisha kuwa tunadumisha mfumo ambapo tunaweza kuwapatia thamani watangazaji na watumiaji pamoja na kuwatuza watayarishi kwa haki na kuwajibika. Matukio ya ulaghai wa kifedha, yanayohusisha kuchuma mapato kwa njia isiyo ya haki kutokana na utazamaji usio halisi au ununuzi kwa kutumia kadi za mikopo zilizoibwa, yanahujumu mfumo huu kwa kuweka hali ya kutoaminiwa na watangazaji, watayarishi na watazamaji.

Tunapotambua matumizi mabaya kama hayo, tunawarejeshea pesa wahusika walioathiriwa vibaya, kama vile watangazaji au watumiaji, panapofaa na inapowezekana. YouTube haiweki akiba ya mapato haya na watayarishi pia hawapaswi kupokea mgao wa mapato yoyote ambayo yamerejeshwa. Hatua zozote tunazoweza kuchukua zinalingana na hali husika, kama ilivyobainishwa katika sera zinazohusiana. Kwa mfano, ingawa tunaweza kujifidia na kurejesha mapato yanayotokana na ulaghai wa kifedha, hatuna nia ya kujifidia mapato ikiwa video zitapatikana baadaye kuwa hazikidhi mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji.

Sehemu ya “Mapato Yasiyotimiza Vigezo” ya sheria na masharti mapya ya Mpango wa Washirika wa YouTube haimaanishi sera mpya. Badala yake, sehemu hii inalenga kuleta uwazi zaidi kuhusiana na sera zetu zilizopo za Mpango kuhusu mabadiliko au kuchelewa kwa malipo katika matukio kama ya ulaghai wa kifedha. Sehemu ya “Mapato Yasiyotimiza Vigezo” inashughulikia hali 2 tofauti ambapo tunaweza kujifidia mapato kukitokea ukiukaji mahususi kama vile chanzo cha hadhira kisicho sahihi:

  1. YouTube inaweza kuzuia au kurekebisha mapato yoyote ya mshirika yanayohusishwa na ukiukaji wa sheria na masharti.
    1. Kwa mfano, tukitambua ulaghai wa kifedha kabla ya malipo kufanywa, huenda tukarekebisha malipo ili kuondoa mapato yanayohusiana au kuzuia malipo ya sehemu hiyo ya mapato huku tukichunguza ulaghai huo.
  2. YouTube inaweza kudai au kukata kiasi hicho kwenye mapato ya mshirika utakayolipwa baadaye.
    1. Kwa mfano, tukitambua ulaghai wa kifedha baada ya kufanya malipo, mapato yanayohusiana yanaweza kukatwa kwenye salio lolote la AdSense katika YouTube ambalo bado halijalipwa au vinginevyo yakatwe kwenye mapato ya baadaye. Hali hii ikitokea, pesa zinazofaa kurejeshwa hukatwa kwenye salio lako la AdSense katika YouTube, si kwenye akaunti yako ya benki.
Hakuna mabadiliko katika jinsi tunavyochakata mapato ya Madai ya Content ID kati ya washirika wanaochuma mapato. Katika hali kama hizi, tutaendelea kuzuia mapato huku dai likiendelea kupingwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
10313291488866747436
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false