Gharama za kuonyesha maudhui katika nchi

Kwa sasa, YouTube haina mpango wa kutekeleza gharama za kuonyesha maudhui katika nchi mnamo mwaka 2023.

Katika baadhi ya nchi duniani kote, usambazaji wa maudhui ya YouTube hutegemea gharama zinazohusiana na mambo kama vile kutoa leseni kwa haki za wahusika wengine, ada za kisheria na kodi za mfumo. Ili kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa shughuli zetu, tunaweza kuanza kugawana na washirika wetu wa kuchuma mapato baadhi ya gharama hizi za kuonyesha maudhui katika nchi.

Kwa sasa hatuna mpango wa kutekeleza gharama hizi mnamo mwaka 2023. Tunapoanza kugawana gharama hizi, tutakuarifu kuhusu gharama zozote zinazotumika kulingana na nchi na jinsi tunavyozihesabu angalau siku 45 kabla. Kwa kuwa gharama hizi zinahusishwa na nchi mahususi, zitakatwa kwa uwiano kulingana na mapato unayopata katika nchi hiyo.

Kumbuka: Ugawanaji wa gharama za kutoa leseni kwa haki za wahusika wengine kupitia gharama za kuonyesha maudhui katika nchi ni tofauti na makato yoyote ya uidhinishaji wa haki za muziki katika marekebisho ya kuidhinisha haki. Kamwe hatutakata gharama za kuonyesha maudhui katika nchi na marekebisho ya kuidhinisha haki ili kulipia gharama za kutoa leseni kwa haki hizohizo.

Jinsi inavyofanya kazi

Utekelezaji wa gharama za kuonyesha maudhui katika nchi unategemea nchi na hutumika katika mifumo yote ya uchumaji wa mapato. Huu hapa ni mfano rahisi dhahania unaomlenga mtayarishi anayepakia video ndefu pekee:

Mfano dhahania

Nchi X imetekeleza kodi ya mfumo ambayo inatumika katika mapato ya utangazaji kwenye YouTube yanayopatikana nchini humo. 

  • Kulingana na mapato ya matangazo marefu ya mshirika katika Nchi X, gharama za kuonyesha maudhui katika nchi imebainishwa kuwa $1. 
  • Baada ya kutekeleza ugavi wa mapato, mshirika atalipa $0.55 na YouTube itagharamia $0.45.
  • Kwa kukata gharama za kuonyesha maudhui katika nchi kabla ya kukokotoa ugavi wa mapato, YouTube na washirika wanagawana gharama hizi kulingana na ugavi wa mapato unaotumika.

Ingawa mfano ulio hapo juu unaonyesha gharama za kuonyesha maudhui katika nchi moja, washirika wanaweza kukumbwa na gharama za kuonyesha maudhui katika nchi nyingi pale mapato ya maudhui yao yanapopatikana katika nchi zaidi ya moja ambamo gharama hizi zinatumika.

Arifa kutoka YouTube

YouTube itakapoanza kugawana gharama hizi, tutakuarifu kuhusu gharama zozote zinazotumika kulingana na nchi na jinsi tutakavyokokotoa gharama angalau siku 45 kabla. Makato yoyote ya gharama za kuonyesha maudhui katika nchi pia yataripotiwa kila mwezi.

Maswali yanayoulizwa sana

Je, gharama za hakimiliki ya muziki zinategemea gharama za kuonyesha maudhui katika nchi?

Hapana. Kugawana gharama za kutoa leseni kwa haki za wahusika wengine kupitia gharama za kuonyesha maudhui katika nchi ni tofauti na makato yoyote ya uidhinishaji wa haki za muziki katika marekebisho ya kuidhinisha haki. Kamwe hatutakata gharama za kuonyesha maudhui katika nchi na marekebisho ya kuidhinisha haki ili kulipia gharama za kutoa leseni kwa haki hizohizo.

Kuchuma mapato katika video zako kupitia muziki bado kunategemea sera zinazotumika za uchumaji mapato za muundo wa video husika. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia Creator Music ukitumia video ndefu na kuchuma mapato katika Video Fupi kupitia muziki.

Je, gharama za kuonyesha maudhui katika nchi zinatumika kulingana na mahali nilipo?

Hapana. Zinahusishwa na nchi mahususi ambapo usambazaji wa maudhui ya YouTube katika nchi hiyo unategemea gharama zinazohusiana na mambo kama vile utoaji wa leseni kwa haki za wahusika wengine, ada za kisheria na kodi za mfumo. Hali hii inamaanisha kuwa gharama hizi zitatumika tu kwa mapato unayopata katika nchi ambamo gharama hiyo ilitekelezwa.

Je, nitajuaje gharama za kuonyesha maudhi katika nchi zinanihusu?

Kwa sasa hatuna mpango wa kutekeleza gharama za kuonyesha maudhui katika nchi mnamo mwaka 2023. Tunapoanza kugawana gharama hizi, tutakuarifu kuhusu gharama zozote zinazotumika kulingana na nchi na jinsi tunavyozihesabu angalau siku 45 kabla. Makato yoyote ya gharama za kuonyesha maudhui katika nchi pia yataripotiwa kila mwezi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12518197178025489088
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false