Kutumia vipengele vya sura na kusogeza

Vidokezo vya kusogeza ili uvinjari maudhui ya YouTube kwenye kifaa chako cha mkononi

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

 

Ukiwa na vipengele vya sura na kusogeza vya YouTube, unaweza kusogeza haraka na kwa urahisi video unayotazama. Usogezaji ni pale unapotumia kisogezaji, nukta nyekundu iliyo kwenye upau wa shughuli, ili kubadilisha sehemu yako katika video.

Kutazama video kulingana na sura

Unaweza kusogeza video kwa kuchagua sura tofauti, ikiwa mtayarishi ameziweka kwenye video yake. Sura hizi hugawa video katika sehemu tofauti.

Ili uende kwenye sura husika:

  1. Bofya video ili ufungue upau wa shughuli. 
  2. Sogeza kisogezaji (nukta nyekundu) hadi kwenye mojawapo ya sura tofauti. Sura zimewekwa alama kwa mstari wima katika upau wa shughuli. Jina la sura litaonekana unaposogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine. 
  3. Bofya cheza  ili uanzishe video kuanzia kwenye sura hiyo. 

Unaweza pia kupata sura kwa kwenda hadi kwenye sehemu ya chini ya maelezo ya video.

Nenda kwenye sehemu za video zilizochezwa tena mara nyingi

Unapoanza kusogeza, grafu hutokea kwenye sehemu ya juu ya upau wa shughuli. Grafu hukuruhusu kupata sehemu za video ambazo hutazamwa tena mara kwa mara. Ikiwa grafu iko juu, basi sehemu hiyo ya video imechezwa tena mara nyingi.

Huenda grafu isionekane juu ya upau wa shughuli kwenye video ikiwa:
  • Kituo kina maonyo ambayo hayajashughulikiwa.
  • Maudhui huenda hayafai.
  • Mifumo yetu imebaini kuwa video haistahiki kwa sababu nyinginezo, kama vile ikiwa video ni mpya mno au imetazamwa mara chache mno.

Usogezaji mahususi

Hali ya usogezaji mahususi hurahisisha kitendo cha kwenda hadi kwenye tukio mahususi katika video.

Use precise seeking to find a specific moment in a video ft. Lyanna Kea 📌 📺

Ili utumie hali ya usogezaji mahususi:

  1. Gusa skrini ili uone upau wa shughuli unaoonekana kwenye skrini.
  2. Telezesha kidole juu kutoka kwenye kisogezaji (nukta nyekundu.)
  3. Utaona safu mlalo yenye vijipicha chini ya upau wa shughuli.

Kuchagua mahali pa kusogezea:

  1. Ukishaona safu mlalo yenye vijipicha, unaweza kuvitelezeshea kidole au kwenye kisogezaji ili urekebishe mkao wa video.
  2. Ili uanze kucheza kuanzia ulipochagua, gusa kitufe cha kucheza au popote pale juu ya vijipicha.
  3. Ili kughairi usogezaji, gusa kitufe cha X.

Kuachilia ili ughairi usogezaji

Wakati unasogeza, unaweza kuamua kutaka kughairi kitendo hiki na urejee ulipoachia kutazama video. Ili ughairi usogezaji:

  1. Hamisha kisogezaji (nukta nyekundu) kwenye upau wa shughuli kuelekea ulipoachia kutazama.
  2. Subiri hadi uhisi mtetemo au uone arifa ya "Achilia ili ughairi".
  3. Inua kidole chako juu ili urudi katika sehemu ulipoachia kutazama kwenye video.
Kumbuka: Kipengele hiki kinapatikana tu kwa programu ya YouTube katika kishikwambi au simu yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12140874596564039224
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false