Kuratibu muda wa kupakia video

Unaweza kutumia uchapishaji ulioratibiwa ili kuratibu video ya faragha ichapishwe kwa umma muda mahususi.

Ratibu video ichapishwe baadaye

Ili uratibu muda wa kuchapisha video, ni sharti kwanza uweke video iwe "imeratibiwa" au "ya faragha" kwenye ukurasa wa kupakia.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
    • Au utumie programu ya YouTube .
  2. Chagua UNDA kisha Pakia video.
  3. Chagua faili ambayo ungependa kupakia na uweke maelezo ya video yako.
  4. Chagua kichupo cha "Uonekanaji", kisha uchague Ratibu.
  5. Weka tarehe, muda na saa za eneo ambazo ungependa video yako ichapishwe.
  6. Chagua Ratibu, Pakia Video fupi, au Pakia video.

Kumbuka: Iwapo akaunti yako ina onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, video yako iliyoratibiwa haitachapishwa katika kipindi cha adhabu. Video yako huwekwa kuwa “faragha” wakati wa kipindi cha adhabu, na inabidi kuiratibu upya kipindi hicho cha kuzuiwa kikiisha. Pata maelezo zaidi kuhusu maelezo ya msingi kuhusu maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.

Badilisha muda ulioratibiwa wa kuchapisha

Unaweza kubadilisha muda ulioratibiwa wa kuchapisha au uchapishe video mara moja.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
    • Au utumie programu ya YouTube .
  2. Kwenye Menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
    • Au uchague picha ya wasifu  kisha Video zako.
  3. Chagua video ambayo ungependa kubadilisha.
  4. Chagua kichupo cha "Uonekanaji":
    • Ili ubadilishe muda ulioratibiwa wa kuchapisha, hakikisha uonekanaji umewekwa kuwa Faragha kisha uchague muda mpya chini ya “Ratibu."
    • Ili uchapishe video mara moja, weka uonekanaji kuwa wa Umma.
  5. Chagua Hifadhi ili uchapishe.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3336003191474863774
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false