Kushiriki Mahali Ulipo na mahali unakochezea kwenye TV

Ili utazame baadhi ya michezo, vipindi na maudhui mengine kwenye Chaneli za YouTube Primetime, unapaswa kuwasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo na kuweka mahali unakochezea. Ni muhimu kuthibitisha mahali ulipo, kwa sababu wakati mwingine maudhui unayoona yanaweza kutegemea mahali ulipo.

Ikiwa tayari umewasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo na unahitaji kusasisha mahali unakochezea, fuata hatua hizi. Ukikumbana na ujumbe wowote kuhusu hitilafu, hatua hizi zinaweza kusaidia.

Unapochagua kipindi cha kutazama kinachohitaji uthibitishaji wa mahali, kama vile mchezo mubashara au ujao kwenye NFL Sunday Ticket, utaona kidokezo kinachokuagiza utumie kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo katika kifaa cha mkononi ili uthibitishe mahali ulipo. Baada ya kukamilika, hatua hii itaweka "mahali unakochezea".

Jinsi ya Kuwasha Kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo ili Utazame Chaneli za Primetime kwenye Televisheni yako

Ikiwa unatumia programu ya YouTube kwenye TV yako, utahitaji TV yako na kifaa chako cha mkononi ili uthibitishe mahali ulipo na uweke mahali unakochezea. Utahitaji uwashe kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye kivinjari chako cha vifaa vya mkononi katika simu au kishikwambi chako. Hali hii itaruhusu programu ya YouTube kwenye TV yako kuthibitisha mahali ulipo.

Kuwasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye kivinjari chako

Ili utazame Chaneli za Primetime, ikiwa ni pamoja na NFL Sunday Ticket, kwenye kompyuta yako, fuata hatua zilizo hapo chini ili uwashe kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo.

  1. Fungua Chrome Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, bofya Menyu  au Zaidi '' kisha bofya Mipangilio.
  3. Bofya Faragha na usalama kisha bofya Mipangilio ya tovuti.
  4. Bofya Mahali kisha uwashe kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwa tovuti mahususi au ruhusu tovuti ziulize mahali ulipo.

Ikiwa umewasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo katika Chrome na video unayojaribu kutazama haitacheza, fungua video kwenye kichupo kipya ili uhakikishe kuwa ruhusa za kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo zimetumika. Ikiwa video bado haitacheza, pata toleo jipya zaidi la Chrome kisha ujaribu tena.

Ikiwa unatumia kivinjari ambacho si Chrome, angalia mipangilio yako ya kivinjari ili ubadilishe ruhusa za mahali. Pata maelezo zaidi kuhusu ruhusa za kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye vivinjari vifuatavyo vya intaneti:

Kuwasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye macOS

Ikiwa hatua zilizo hapo juu hazifanyi kazi, hakikisha macOS yako ni toleo la 13.5.1 au toleo jipya zaidi. Ili upate toleo jipya la macOS yako:
 
Fungua menyu ya Apple  kisha bofya Mipangilio ya Mfumo kisha bofya Jumla kisha bofya Sasisho la Programu.

Ili uwashe kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye programu katika macOS:

  1. Fungua menyu ya Apple  kisha bofya Mipangilio ya Mfumo kisha bofya Faragha na Usalama kisha bofya Huduma za Mahali.
  2. Bofya kitufe cha kuwasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye kivinjari chako. Kitufe kitabadilika na kuwa cha bluu.

Kuthibitisha au kubadilisha mahali unakochezea kwenye TV yako

Baada ya kuwasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye kivinjari chako cha kifaa cha mkononi, chagua maudhui ya kutazama katika TV yako. Iwapo utapokea ujumbe wa 'thibitisha mahali unakochezea sasa', fuata hatua hizi:

  1. Nenda kwenye youtube.com/locate katika kivinjari cha kifaa cha mkononi kisha ingia katika akaunti hiyo ya Google uliyotumia kuingia katika televisheni au kifaa chako cha kutiririsha. 
    • Kidokezo: Anwani ya barua pepe ya akaunti yako inapaswa kuonyeshwa kwenye skrini ya TV yako chini ya Mipangilio kisha Ununuzi na Uanachama.
  2. Baada ya kuingia katika akaunti, unapaswa uone dirisha ibukizi ili uwashe kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwenye kivinjari chako. Gusa INAYOFUATA kisha Ruhusu.
  3. Onyesha upya ukurasa wa youtube.com/locate katika kifaa chako cha mkononi kisha ondoka na ufungue tena programu kwenye televisheni yako.

Iwapo huoni sasisho likifanywa kwenye TV yako, kagua ili uhakikishe kwamba umeingia katika akaunti sahihi kwenye kivinjari cha kifaa cha mkononi na TV yako. Baadaye, jaribu kuondoka na kufungua tena programu kwenye TV yako. Ikiwa bado hatua hizi hazifanyi kazi, jaribu kufuta akiba na vidakuzi vyako kisha ujaribu tena.

Kutatua ujumbe kuhusu hitilafu kama vile 'Usasishaji wa eneo haupatikani'
Ikiwa unaona ujumbe kuhusu hitilafu “Washa ruhusa za mahali za kivinjari” au “Usasishaji wa eneo haupatikani”, jaribu hatua hizi:
  1. Thibitisha kuwa kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kimewashwa kwenye kifaa chako cha mkononi na kivinjari cha kifaa cha mkononi kwa hatua zilizo hapo juu.
  2. Hakikisha kuwa unatumia kifaa cha mkononi na si kompyuta ili ufuate hatua kwenye youtube.com/locate.
  3. Ondoka na ufungue tena programu ya YouTube kwenye TV yako kisha ujaribu tena.
  4. Thibitisha kuwa vifaa vya mkononi na TV yako imesasishwa kwa kuangalia toleo katika mipangilio yako.
  5. Futa akiba na vidakuzi kwenye kifaa chako cha mkononi kisha ujaribu tena.

Kutatua kutuma maudhui

Ikiwa una tatizo lolote la kuthibitisha mahali ulipo unapotuma maudhui, jaribu:

  • Kutuma upya na kufuata hatua zilizo hapo juu.
  • Kufuta akiba na vidakuzi vya kivinjari chako (kwenye youtube.com) kisha utume maudhui tena.
  • Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti ile ile uliyotumia kwenye programu ya YouTube katika kifaa cha mkononi na programu ya YouTube kwenye TV yako.

Kuwasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo kwa ajili ya kutuma maudhui kwenye TV yako

Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti ile ile kwenye kifaa cha mkononi na programu yako ya YouTube katika TV yako na umewasha kipengele cha Kushiriki Mahali Ulipo katika kivinjari cha kifaa cha mkononi na programu yako ya YouTube kwa kufuata hatua zilizo hapo juu. Kisha:

  1. Fungua programu kwenye kifaa chako cha mkononi na utume maudhui  ya kipindi katika TV yako.
  2. Fuata vidokezo katika programu ya YouTube kwenye televisheni yako. 
  3. Fungua youtube.com/locate kwenye kivinjari cha kifaa cha mkononi ukitumia akaunti sawa uliyoingia katika programu ya YouTube. 
  4. Televisheni yako inapaswa ianze kucheza kiotomatiki baada ya data ya mahali kutolewa kwenye kifaa chako cha mkononi.
Kusasisha mahali unakochezea katika televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti ikiwa si sahihi
Baada ya mahali unakochezea kuhifadhiwa kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, ukibaini kuwa si sahihi, unaweza kubadilisha au kufuta data yake kwa kwenda katika mipangilio kwenye kifaa chako:
  1. Fungua programu ya YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.
  2. Nenda kwenye Mipangilio kisha Mahali unakochezea.
  3. Badilisha mahali ulipo:
    • Chagua penseli ili ubadilishe na uweke msimbo wako wa eneo.
    • Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili uweke na uthibitishe Mahali unakochezea sasa.

Kufuta Mahali unakochezea kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

Ili ufute Mahali unakochezea:

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye televisheni yako.
  2. Nenda kwenye Mipangilio kisha Futa data ya mahali unakochezea.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9891006413301616398
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false