Muhtasari wa Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube

Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube huwapatia watayarishi fursa ya kukutana, kuwasiliana na kujifunza kutoka kwa watayarishi wengine watakaoshirikiana nao kwenye YouTube. Watayarishi pia watapata usaidizi kutoka kwa Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya YouTube (CPM), atakayewapatia mwongozo wa kutumia YouTube.

Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya YouTube ni nani?

Lengo la Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya YouTube ni kuunda jumuiya inayoelimisha, kuhamasisha na kuboresha hali za utumiaji za watayarishi. Hii inaweza kutoa ufikiaji wa fursa zinazoboresha mawasiliano ya watayarishi, kuwaongoza kwenye YouTube na kuwawezesha wasimamie hali zao za utumiaji kwenye YouTube.

Hizi ni baadhi tu ya njia chache za jinsi ambavyo CPM wanaweza kuwasaidia watayarishi wafanikiwe kwenye YouTube:

  • Kuwapatia uwezo wa kuwasiliana na watayarishi wanaohamasisha
  • Kutoa masasisho ya mara kwa mara kuhusu Mbinu Bora, vipengele na vidokezo vipya
  • Kutoa mialiko ya kipekee ya warsha na matukio ya watayarishi au ya sekta
  • Kutoa matoleo ya Beta ya vipengele vipya vya bidhaa, uzinduzi na elimu kuhusu vipengele vipya
  • Kutoa fursa ya kutuma maoni moja kwa moja kwa Timu za bidhaa

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube

Ni nani anaweza kujiunga na Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube?

Jumuiya yetu ya Watayarishi wa YouTube ni ya walioalikwa pekee, hivyo angalia Studio ya YouTube au barua pepe yako mara kwa mara ili upate maelezo kuhusu kujiunga. Nafasi za kujiunga na Jumuiya ya Watayarishi ni chache na Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya watawasiliana na watayarishi waliokubaliwa ili kuwaeleza hatua zinazofuata.

Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube inalenga watayarishi wanaochapisha mara kwa mara na ni mahususi kwa chaneli zinazotii Mwongozo wetu wa Jumuiya. Ikiwa watayarishi hawatimizi tena masharti ya kujiunga au wanakiuka mwongozo wetu wa jumuiya, wanaweza kupoteza uwezo wa kufikia Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube.

Kwa ujumla, tunafanya kazi na chaneli ambazo:

  • Zinapatikana au kulenga nchi au maeneo ambako Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya wanapatikana
  • Zinachapisha mara kwa mara kwenye YouTube
  • Zina uwezekano wa kukua
  • Havina maonyo yoyote kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya
  • Hazina zaidi ya onyo moja la hakimiliki ambalo halijatatuliwa
  • Zinafuata mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji
  • Zinawaheshimu Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya pamoja na watayarishi wote wanaoshiriki wakati wanahudhuria warsha, matukio ya Jumuiya na shughuli nyinginezo kama hizo

Je, ni nchi na maeneo gani yanatimiza masharti ya kujiunga na Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube?

  • Albania
  • Ajentina
  • Australia
  • Austria
  • Bahareni
  • Bangladeshi
  • Ubelgiji
  • Bolivia
  • Bosnia na Hezegovina
  • Brazili
  • Bulgaria
  • Kanada
  • Chile
  • Kolombia
  • Kostarika
  • Korasia
  • Kuba
  • Jamhuri ya Zechia
  • Denmaki
  • Jamhuri ya Dominika
  • Ekwado
  • Misri
  • Elsavado
  • Estonia
  • Ufini
  • Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ghana
  • Gwatemala
  • Hondurasi
  • Hangaria
  • India
  • Indonesia
  • Iraki
  • Ayalandi
  • Japani
  • Yordani
  • Kenya
  • Kuwaiti
  • Lativia
  • Lebanoni
  • Libya
  • Lithuania
  • Lasembagi
  • Masedonia
  • Malesia
  • Meksiko
  • Moldova
  • Montenegro
  • Moroko
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Nikaragua
  • Nigeria
  • Norwe
  • Omani
  • Pakistani
  • Panama
  • Paragwai
  • Peru
  • Ufilipino
  • Polandi
  • Pwetoriko
  • Katari
  • Romania
  • Saudia
  • Sabia
  • Singapoo
  • Slovenia
  • Afrika Kusini
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Thailandi
  • Tunisia
  • Uturuki
  • Muungano wa Falme za Kiarabu
  • Uingereza
  • Marekani
  • Urugwai
  • Venezuela
  • Vietnamu

Je, Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya YouTube anatozwa gharama zozote?

Hapana, unapata huduma ya kuwa Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya bila kulipia.

Je, Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ni tofauti na Msimamizi wa Washirika?

Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya wanaosimamia Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube pamoja na Mpango wa Wasimamizi wa Washirika wa YouTube ni mipango miwili tofauti yenye vipengele vya huduma na vigezo mahususi vya uteuzi.

Jumuiya ya Watayarishi wa YouTube husimamia Jumuiya kubwa ambako watayarishi wanaweza kuwasiliana na watayarishi wengine. Mpango wa Wasimamizi wa Washirika huhudumia watayarishi mahususi kama wataalamu binafsi wa YouTube wanaotoa usaidizi wa ana kwa ana.

Nimegundua kuwa sistahiki. Ninapaswa kuchukua hatua gani?

Usiwe na wasiwasi! Kuna nyenzo nyingi ambazo bado unaweza kutumia ili kukuza chaneli yako:

Je, nitajuaje kwamba barua pepe ninazopokea kwa hakika zinatoka YouTube?

Tunafahamu kuwa watayarishi hupata barua pepe nyingi kuhusu vituo vyao. Hivi ndivyo unavyoweza kuangalia iwapo barua pepe imetoka kwenye timu ya YouTube:

  • Angalia kikoa cha barua pepe: Hakikisha kwamba barua pepe inatoka kwenye anwani ya barua pepe yenye kikoa cha @google.com, @youtube.com au @partnerships.withyoutube.com. Barua pepe zinazotoka kwenye vikoa vingine vyovyote ambazo zinadai kutoka YouTube or Google zinaweza kuwa bandia.
  • Angalia viungo: Hakikisha kuwa URL za viungo au fomu zilizojumuishwa kwenye barua pepe zinaishia na youtube.com, withgoogle.com, withyoutube.com, youtube.secure.force.com, au youtube.force.com.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
526440346159249388
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false