Jiunge na Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube

Watayarishi walio katika Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube hupata uwezo wa kufikia Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube (CPM), anayewaongoza katika masuala ya Video Fupi.

Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube ni nani?

Lengo la Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube ni kuelimisha, kuhamasisha na kukuza Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi – kutoa ufikiaji kwa fursa zinazopanua mitandao ya watayarishi, kuwaongoza watayarishi kwenye YouTube na Video Fupi na kuwawezesha watayarishi kumiliki hali yao ya matumizi ya YouTube.

Hizi ni baadhi ya njia chache tu ambazo CPM wa Video Fupi za YouTube wanaweza kuwasaidia watayarishi kufanikiwa kwenye YouTube:

 • Kuwapa uwezo wa kufikia mtandao unaoendelea kupanuka wa watayarishi hodari
 • Kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu Mbinu Bora za Video Fupi, vipengele vipya na vidokezo
 • Kutoa mialiko ya matukio ya watayarishi/sekta na warsha
 • Kufikia toleo la Beta la vipengele vipya vya bidhaa, uzinduzi na elimu kuhusu vipengele vipya vya Video Fupi
 • Kupata fursa ya kushiriki maoni moja kwa moja na timu ya Video Fupi

Ni nani anayeweza kujiunga na Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube?

Jumuiya ya CPM ya Video Fupi za YouTube inawalenga watayarishi wanaochapisha mara kwa mara na hutolewa kwa vituo vinavyotimiza Mwongozo wetu wa Jumuiya. Watayarishi wa Video Fupi katika Jumuiya wanaweza pia kuendelea kuwepo katika jumuiya mradi wanaendelea kutayarisha Video Fupi na kufuata masharti ya kujiunga. Iwapo Watayarishi wa Video Fupi hawatayarishi Video Fupi mara kwa mara au hawatimizi masharti yetu ya kujiunga, wanaweza kupoteza uwezo wa kufikia Jumuiya.

Kwa ujumla, tunafanya kazi na vituo ambavyo:

 • Vinapatikana au vinalenga nchi/maeneo ambapo Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Video Fupi za YouTube wanapatikana
 • Vimejikita katika utayarishaji wa video fupi kwa chaguomsingi
 • Vinachapisha mara kwa mara kwenye Video Fupi
 • Vina uwezekano wa kukua
 • Havina maonyo yoyote kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya
 • Havina zaidi ya onyo moja la hakimiliki ambalo halijatatuliwa
 • Vinatii masharti ya Hazina ya Video Fupi
 • Vinafuata mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji
 • Vinaheshimu watayarishi wote wanaoshiriki na Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya wakati wanahudhuria matukio, warsha na matukio mengine

Jumuiya yetu ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube ni ya walioalikwa pekee. Ili utume maombi ya kupokea mwaliko, nenda kwenye ukurasa wetu katika tovuti ya Watayarishi wa YouTube.

Pata maelezo zaidi kuhusu Jumuiya ya Video Fupi za YouTube

Ni nchi/maeneo yapi yanastahiki kushiriki katika Jumuiya ya CPM ya Video Fupi za YouTube?

 • Ajentina
 • Australia
 • Austria
 • Bahareni
 • Ubelgiji
 • Bolivia
 • Brazili
 • Kanada
 • Chile
 • Kolombia
 • Kostarika
 • Kuba
 • Denmaki
 • Jamhuri ya Dominika
 • Ekwado
 • Misri
 • Elsavado
 • Ufini
 • Ufaransa
 • Ujerumani
 • Ghana
 • Gwatemala
 • Hondurasi
 • India
 • Indonesia
 • Iraki
 • Ayalandi
 • Japani
 • Yordani
 • Kenya
 • Kuwaiti
 • Lebanoni
 • Libya
 • Lasembagi
 • Malesia
 • Meksiko
 • Moroko
 • Nikaragwa
 • Naijeria
 • Norwe
 • Omani
 • Pakistani
 • Panama
 • Paragwai
 • Peru
 • Ufilipino
 • Pwetoriko
 • Katari
 • Saudia
 • Singapoo
 • Afrika Kusini
 • Korea Kusini
 • Uhispania
 • Uswidi
 • Uswizi
 • Tailandi
 • Uholanzi
 • Tunisia
 • Uturuki
 • Muungano wa Falme za Kiarabu
 • Uingereza
 • Marekani
 • Urugwai
 • Venezuela
 • Vietinamu

Kuna gharama yoyote ya kuwa na Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube?

Hapana, kuwa na Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube ni huduma unayopata bila malipo yoyote.

Je, Msimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube ni tofauti na Msimamizi wa Washirika?

Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube (CPM) na Mpango wa Wasimamizi wa Washirika wa YouTube ni mipango miwili tofauti yenye vigezo na vipengele vya huduma tofauti.

Wasimamizi wa Washirika wa Jumuiya ya Watayarishi wa Video Fupi za YouTube (CPM) hudhibiti Jumuiya kubwa ya Watayarishi chipukizi wa Video Fupi. Mpango wa Wasimamizi wa Washirika husaidia watayarishi binafsi kama wataalamu binafsi wa kuwasiliana nawe ana kwa ana kwenye YouTube.

Nimegundua kuwa sistahiki. Ninapaswa kuchukua hatua gani?

Usiwe na wasiwasi! Kuna nyenzo nyingi ambazo bado unaweza kuzitumia kukuza kituo chako:

Nitajuaje kwamba barua pepe ninazopokea zinatoka YouTube?

Tunafahamu kuwa watayarishi hupata barua pepe nyingi kuhusu vituo vyao. Hivi ndivyo unavyoweza kuangalia iwapo barua pepe imetoka kwenye timu ya YouTube:

 • Angalia kikoa cha barua pepe: Hakikisha kwamba barua pepe inatoka kwenye anwani ya barua pepe yenye kikoa cha @google.com, @youtube.com au @partnerships.withyoutube.com. Barua pepe zinazotoka kwenye vikoa vingine vyovyote, ambazo zinadai kutoka kwenye YouTube or Google zinaweza kuwa bandia.
 • Angalia viungo: Hakikisha kuwa URL za viungo au fomu zilizojumuishwa kwenye barua pepe zinaisha kwa youtube.com, withgoogle.com, withyoutube.com, youtube.secure.force.com, or youtube.force.com.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu