Kumwalika mgeni kwenye mtiririko wako mubashara kupitia kipengele cha Peperusha Mubashara Pamoja

Watayarishi wanaotimiza masharti wanaweza kumwalika mgeni atiririshe mubashara pamoja nao. Ukitumia simu ya mkononi kutiririsha mubashara, mipasho ya mtiririko wako mubashara itaonekana karibu na mipasho ya mgeni wako.

Unaweza kuratibu mtiririko mubashara pamoja na mgeni kwenye kompyuta yako (kupitia Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja) kisha utiririshe mubashara kwenye simu yako ya mkononi. Au unaweza kutiririsha mubashara kwenye simu yako ya mkononi.

 

Peperusha Mubashara Pamoja na mgeni

Unaweza kuwazungusha wageni kwenye mtiririko wako mubashara, ingawa unaweza tu kuwa na mgeni mmoja anayeonekana kwenye mtiririko wako mubashara kwa wakati mmoja. Unaweza kuona takwimu za mtiririko wako mubashara ndani ya Studio ya YouTube, lakini mgeni wako hawezi.

  1. Kwenye simu yako, fungua programu ya YouTube.
  2. Kwenye sehemu ya chini, gusa Buni + Peperusha Mubashara Pamoja.
  3. Weka maelezo ya mtiririko, ikiwa ni pamoja na mada, ufafanuzi, mipangilio ya uchumaji wa mapato, mipangilio ya vijipicha na ya uonekanaji.
  4. Gusa Nimemaliza.
  5. Katika sehemu ya “Alika mtiririshaji mwenza,” teua chaguo la kumwalika mgeni wako:
    • Nakili kiungo: Nakili kiungo na ukitume kwa mgeni wako katika ujumbe wa maandishi, barua pepe au kwenye jukwaa la kijamii unalopenda. 
    • Tuma kiungo cha mwaliko kwa mtiririshaji mwenza: Chagua mfumo wa kutuma ujumbe unaopendelea ili utume kiungo cha mwaliko. 
  6. Mgeni wako atabofya kiungo na ataelekezwa kwenye sehemu ya kusubiri.
  7. Ukiwa tayari, gusa Tiririsha Mubashara.
  8. Wakati mtiririshaji mwenza anajiunga kwenye sehemu ya kusubiri, utaona arifa. Chagua Weka kisha Tiririsha mubashara ili uanzishe mtiririko wako mubashara.
  9. Video yako itaonekana karibu na mgeni wako na mkao chaguomsingi utakuwa wima.
Kumbuka: Unaweza kumwalika mtu mwingine aliye na chaneli ya YouTube atiririshe pamoja nawe. Hahitaji kuwa Mchunguzaji Mwaminiwa. Unaweza kuwazungusha wageni kwenye mtiririko wako mubashara, ingawa unaweza tu kuwa na mgeni mmoja anayeonekana kwenye mtiririko wako mubashara kwa wakati mmoja. Unaweza kuona Takwimu za mtiririko wako mubashara ndani ya Studio ya YouTube, lakini mgeni wako hawezi.

Jiunge katika mtiririko kama mgeni

Unaweza kutiririsha pamoja na mtu mwingine kwa kualikwa ujiunge kwenye mtiririko wake mubashara. Kutiririsha pamoja na mtu mwingine kunaweza kukusaidia uwasiliane na hadhira mpya kwenye YouTube.

  1. Gusa kiungo cha mwaliko kilichotumwa na mwenyeji anayetiririsha mubashara kwenye kifaa chako cha mkononi. Anaweza kukutumia kupitia barua pepe, ujumbe au huduma nyingine ya kutumiana ujumbe.
  2. Chagua kituo ambacho ungependa kutumia kutiririsha mubashara.
  3. Chagua Jiunge unapoulizwa ujiunge kwenye sehemu ya kusubiri.
  4. Unaposubiri kutiririsha mubashara, angalia ubora wa sauti na video yako.
  5. Unapoona “Unatiririsha mubashara,” sasa unatiririsha pamoja na mwingine kwenye YouTube.

Maswali yanayoulizwa sana

Je, matangazo yanaweza kuonekana kwenye mtiririko wa Peperusha Mubashara Pamoja na kituo cha mwenyeji kitachuma mapato?

Ndiyo, matangazo yanayoonyeshwa kabla, katikati na baada ya video huonekana kwenye mitiririko ya Kupeperusha Mubashara Pamoja na yatahusishwa na kituo cha mwenyeji cha mtiririko husika.

Nini kitafanyika iwapo mgeni atakiuka sera ya YouTube, kwa mfano, Mwongozo wa Jumuiya au sera ya hakimiliki, wakati wa mtiririko mubashara?

Kituo kinachopangisha kinawajibikia maudhui yote ya moja kwa moja na kinapaswa kuhakikisha kuwa wageni na maudhui yote yatatii sheria na masharti yetu ya YouTube, ikiwa ni pamoja na Mwongozo wetu wa Jumuiya, sera ya hakimiliki na sera zingine zote zinazotumika. Kwa mfano, mgeni akikiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye mtiririko, kituo kinachopangisha kitawajibikia hali hiyo. Kabla ya kutiririsha mubashara, mwelimishe mtiririshaji mwenza kuhusu anachoweza kufanya na asichoweza kufanya. Mwenyeji atapata zana za udhibiti wakati wa mtiririko mubashara na ataweza kumwondoa mtiririshaji mwenza wakati wowote.

Nilibuni kiungo cha kumwalika mtiririshaji mwenza. Ninawezaje kukibadilisha?

Buni au ubadilishe mtiririko mubashara kisha uende kwenye “Alika mtiririshaji mwenza.” Kwenye sehemu ya chini, bofya Badilisha Kiungo. Kiungo cha awali hakitamruhusu mtu kujiunga kwenye mtiririko wako. Tuma kiungo hicho kipya kwa mtiririshaji wako mwenza.

Nimetuma kiungo ili kumwalika mtiririshaji mwenza lakini hawezi kujiunga. Ninapaswa kuchukua hatua gani?

Wakati mwingine programu fulani za kutuma ujumbe hazifungui kiungo cha mwaliko ipasavyo. Katika hali hizi, tunapendekeza watayarishi watume tena kiungo kupitia barua pepe au ujumbe wa maandishi. Pata maelezo zaidi hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9047747221356408434
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false