Ukitumia kipengele cha Upakuaji wa kiotomatiki, video zinazopendekezwa huwekwa kiotomatiki kwenye vipakuliwa vyako ili utazame nje ya mtandao. Tazama video popote ulipo na ugundue maudhui mapya bila ugumu wa kutafuta. Upakuaji utakomeshwa ukitenganisha mtandao wa Wi-Fi au nafasi ya hifadhi ya kifaa chako ikikaribia kujaa.
How to download videos with YouTube Premium
Kuwasha Upakuaji wa kiotomatiki
Kutoka kwenye akaunti ya YouTube Premium ambako umeingia.
- Fungua programu ya YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Vipakuliwa
.
- Kwenye Menyu
, chagua Mipangilio.
- Geuza ili uwashe Upakuaji wa kiotomatiki
.
Kumbuka: Ni sharti kifaa chako kiunganishwe kwenye intaneti ili uanze kupakua video.
Kuzima Upakuaji wa kiotomatiki
Kutoka kwenye akaunti ya YouTube Premium ambako umeingia.
- Fungua programu ya YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Vipakuliwa
.
- Kwenye Menyu
, chagua Mipangilio.
- Geuza ili uzime Upakuaji wa kiotomatiki
.
Kupata na kutazama maudhui ya Upakuaji wa kiotomatiki
Kutoka kwenye akaunti ya YouTube Premium ambako umeingia.
- Fungua programu ya YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Vipakuliwa
Upakuaji wa Kiotomatiki.
Utaona orodha ya video zinazopendekezwa zilizochaguliwa na kupakuliwa kwa ajili yako kulingana na historia ya video ulizotazama.
Kuondoa video kwenye kipengele cha Upakuaji wa Kiotomatiki
Ondoa vipakuliwa vinavyopendekezwa katika njia mbili:
- Chini ya kicheza video, gusa Zilizopakuliwa
kando ya video ambayo ungependa kuondoa.
- Bofya Futa.
Au
- Gusa picha yako ya wasifu
Vipakuliwa
.
- Gusa Menyu
karibu na video ambayo ungependa kuiondoa.
- Chagua Futa kwenye vipakuliwa.
Video mpya zitapakuliwa kila baada ya siku 7 na video zilizopakuliwa awali zitabadilishwa.
Kubadilisha ubora wa Upakuaji wa kiotomatiki
Kutoka kwenye akaunti ya YouTube Premium ambako umeingia.
- Fungua programu ya YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Vipakuliwa
.
- Kwenye Menyu
, chagua Mipangilio.
- Gusa Ubora wa kupakua.
- Chagua mipangilio ya ubora wa kupakua unaopendelea kwenye chaguo zilizoorodheshwa hapa chini.
Rekebisha mipangilio yako ya nafasi ya hifadhi
Kutoka kwenye akaunti ya YouTube Premium ambako umeingia.
- Fungua Programu ya YouTube na uende kwenye Mipangilio yako.
- Gusa Chinichini na vipakuliwa
Upakuaji wa kiotomatiki.
- Nenda kwenye Matumizi ya nafasi ya hifadhi
Maalum.
- Tumia kitelezi ili uchague kiasi cha nafasi ya hifadhi ambacho ungependa kifaa chako kitumie kwa ajili ya Upakuaji wa kiotomatiki.