Kutazama video nje ya mtandao ukitumia YouTube Premium

Ikiwa YouTube Premium inapatikana katika eneo ulipo, unaweza kupakua na kutazama video kwenye kifaa chako cha mkononi. Unaweza pia kupakua video kwenye kompyuta yako ukitumia vivinjari vya Chrome, Edge, Firefox na Opera. Tunatarajia kujumuisha kipengele hiki kwenye vivinjari vingine katika siku zijazo.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti mipangilio yako ya kupakua ukitumia YouTube Premium au kujisajili ili upate YouTube Premium ili uanze.

Pakua video ili utazame nje ya mtandao

Ili upakue video kwenye kompyuta yako:

  1. Tembelea youtube.com kwenye akaunti yako ya YouTube Premium ambayo umetumia kuingia.
  2. Nenda kwenye Ukurasa wa kutazama wa video ambayo ungependa kuipakua.
  3. Chini ya video hiyo, bofya Pakua .

Baada ya video kupakuliwa, aikoni ya kupakua itabadilika kuwa nyeusi chini ya video hiyo .

Kifaa chako kikipoteza muunganisho wa intaneti wakati wa kupakua video, shughuli hiyo itaendelea kiotomatiki muunganisho wako wa intaneti ukirudi tena.

Tazama video ulizozipakua

Ili upate na utazame video ambazo umezipakua kwenye kompyuta yako:

  1. Tembelea youtube.com kwenye akaunti yako ya Premium uliyotumia kuingia.
  2. Bofya Zilizopakuliwa kwenye menyu ya kushoto.

Ondoa video mahususi kwenye orodha ya zile ulizozipakua

Unaweza kuondoa video ulizopakua kwa njia mbili:

  1. Chini ya kicheza video, gusa Zilizopakuliwa karibu na video ambayo ungependa kuiondoa.
  2. Bofya Futa.

Au

  1. Nenda kwenye ukurasa wako wa Zilizopakuliwa .
  2. Chagua Zaidi '' karibu na video ambayo ungependa kuiondoa.
  3. Bofya Ondoa kwenye zilizopakuliwa.
  4. Bofya Futa kwenye kidirisha kilicho chini ya "Ungependa kufuta zote zilizopakuliwa?"

Ondoa video zote ulizozipakua

Unaweza kuangalia na ufute video ambazo umezipakua kwa kufuata hatua hizi:

  1. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Zilizopakuliwa.
  2. Gusa Mipangilio ya Zilizopakuliwa kisha Futa zote zilizopakuliwa.
  3. Bofya Futa kwenye kidirisha kilicho chini ya "Ungependa kufuta zote zilizopakuliwa?"

Sasisha mipangilio ya kupakua

Weka ubora chaguomsingi wa video zako zilizopakuliwa kwa kwenda kwenye Mipangilio kisha Zilizopakuliwa kisha Ubora wa kupakua.

Video za ubora wa juu zaidi zinaweza kutumia data zaidi, kuchukua muda mrefu zaidi kuonekana katika sehemu ya Vipakuliwa na kutumia nafasi zaidi kwenye kifaa chako.

Kutatua matatizo wakati wa kupakua video

  • Video zilizopakuliwa zinaweza kuchezwa nje ya mtandao kwa kipindi cha siku 29. Baada ya muda huo, utahitaji kuunganisha upya kifaa chako kwenye intaneti. Hatua ya kuunganisha upya itaruhusu programu kuangalia iwapo kuna mabadiliko kwenye video au upatikanaji wake. Ikiwa video haiwezi kuchezwa tena nje ya mtandao, itaondolewa kwenye kifaa chako wakati wa usawazishaji ujao.
  • Katika baadhi ya nchi au maeneo, maudhui yanaweza kuchezwa kwa hadi saa 48 bila muunganisho wa intaneti. Unapaswa kuingia katika akaunti yako ya Premium ili upakue video. Video zilizoongezwa kwenye video zako zilizopakuliwa zinaweza kucheza ukiwa umeingia katika akaunti ile moja. Baadhi ya vipengele, kama vile kutoa maoni na kupenda, vinapatikana tu wakati kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao wa Wi-Fi. Pata maelezo zaidi kuhusu video za nje ya mtandao za YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2131591371792130854
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false