Ili ugundue video ambazo hadhira na watazamaji wako wanatafuta kwenye YouTube, unaweza kutumia Kichupo cha Zinazovuma. Maarifa kutoka kwenye Kichupo cha Zinazovuma yanaweza kukusaidia kupata mawazo kuhusu video yako ijayo.
Kuanza kutumia Kichupo cha Zinazovuma
Kumbuka: Kwa sasa, baadhi ya maarifa yanapatikana tu katika nchi, lugha na vifaa fulani. Ikiwa hakuna video zinazofaa kwa sasa, huenda usione baadhi ya sehemu.
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Katika menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
- Kwenye menyu ya juu, bofya kichupo cha Zinazovuma .
- Ili uanze, unaweza kugundua yaliyo kwenye ukurasa wa zinazovuma au kuweka mada ya utafutaji kwenye upau wa kutafutia. Ili uhifadhi hoja ya utafutaji, bofya Hifadhi.
Kugundua Kichupo cha Zinazovuma
Utafutaji maarufu
Kadi hii huonyesha utafutaji maarufu kulingana na hadhira yako na hoja za utafutaji ulizohifadhi katika siku 28 zilizopita.
Video zenye kipaumbele
Kadi hii huangazia maudhui yenye utendaji wa juu kutoka kwa watayarishi wengine walio na chaneli zenye maudhui sawa na yako. Haya husaidia kukupa mawazo yanayosisimua ya kutumia katika video yako ijayo itakayoifaa hadhira yako.
Video za hivi majuzi
Kadi hii huonyesha video zinazohusiana na mada ambazo hadhira yako ilitazama katika siku 28 zilizopita na mada za utafutaji ulizohifadhi.
Upungufu wa maudhui kwenye Video Fupi
Kadi hii huonyesha hoja za utafutaji za Video Fupi zinazohusiana na mada ambazo hadhira yako ilitazama katika siku 28 zilizopita pamoja na mada za utafutaji ulizohifadhi.
Kutafuta kwenye Kichupo cha Zinazovuma
Mambo yanayovutia hadhira
Huenda ukaona kiwango cha kuvutiwa cha hadhira yako kwenye utafutaji na mapendekezo unapotafuta mawazo mapya kuhusu video. Mambo haya yanayovutia hadhira hulingana na video zilizotazamwa zaidi ya mara 1000 kwa wiki na kuanzia siku 28 zilizopita. Kiwango hiki cha kuvutiwa huanza cha chini zaidi hadi cha juu zaidi.
Zinazotazamwa kwenye YouTube
Hii huonyesha video maarufu za mada husika zilizotazamwa na watazamaji kwenye YouTube.
Zinazotafutwa kwenye YouTube
Kadi hii huonyesha utafutaji maarufu kulingana na hadhira yako na hoja za utafutaji ulizohifadhi katika siku 28 zilizopita.
Unaweza kugundua upungufu wa maudhui kwa kuchagua Onyesha upungufu zaidi wa Maudhui. Hii huonyesha Upungufu wa maudhui ambapo watazamaji huenda wanatafuta Video Fupi zinazofaa au zenye ubora wa juu zaidi.
Pata maelezo kuhusu Upungufu wa maudhui
Upungufu wa maudhui hutokea watazamaji wanaposhindwa kupata matokeo bora na ya kutosha ya utafutaji wa mada mahususi wanayotafuta kwenye YouTube. Unaweza kutumia upungufu wa maudhui kama msukumo wa kutayarisha maudhui ambayo hayapo au yanayoweza kuboreshwa.
Upungufu wa maudhui unaweza kutokea wakati:
- Watazamaji hawawezi kupata matokeo yoyote ya utafutaji wao.
- Watazamaji hawawezi kupata maudhui yanayolingana kabisa na utafutaji wao.
- Watazamaji hawawezi kupata video zinazofaa kwa utafutaji wao, kwa mfano maudhui ni ya zamani au yana ubora duni.