|
Mwongozo wa chaneli unaonyesha aina ya mazungumzo ambayo ungependa yawe kwenye chaneli yako. Watazamaji watapata mwongozo wa chaneli yako kabla ya kutoa maoni kwenye video, chapisho katika Jumuiya yako au wakati wa gumzo lako la moja kwa moja. Ili uanze:
Mwongozo wako maalum hautasababisha maoni, machapisho wala ujumbe wa gumzo la moja kwa moja kuondolewa au kufichwa kiotomatiki. Badala yake utakusaidia kuweka matarajio kuhusu maoni ambayo wewe au wadhibiti wa chaneli yako mnaweza kuzuilia. Ingawa YouTube haitatekeleza kiotomatiki mwongozo wako maalum, tutaendelea kutekeleza kiotomatiki Mwongozo wetu wa Jumuiya. |
Pata maelezo zaidi kuhusu mwongozo wa chaneli
Nitasema nini katika ujumbe wangu wa makaribisho na mwongozo wa chaneli?
Huenda wanaotazama chaneli yako kwa mara ya kwanza wasiifahamu wanapotoa maoni kwenye video zako, kuchapisha au kushiriki katika magumzo ya moja kwa moja. Andika ujumbe wa makaribisho kwa hadhira yako na kuihimiza ifuate mwongozo wako. Kwa mfano, unaweza kuandika: “Karibu kwenye chaneli yangu! Tafadhali fuata mwongozo wa chaneli yangu unapojiunga kwenye mazungumzo.”
Mwongozo wako huwafahamisha watazamaji jinsi ya kuwasiliana kwenye chaneli yako. Andika mwongozo unaohimiza aina za mazungumzo ambayo ungependa yafanywe kwenye chaneli yako. Mifano ya amri nzuri ni pamoja na:
- Kuwa na adabu na heshima
- Kuandika maoni kuhusu mada pekee
- Maswali yanaruhusiwa
- Hamna taka au kujitangaza
- Pinga maoni, si mtu