Kuanza kutumia kipengele cha Muziki wa Watayarishi

Kipengele cha Muziki wa Watayarishi sasa kinapatikana kwa watayarishi wa Marekani walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP). Upanuzi kwa watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube nje ya Marekani unashughulikiwa.
Kumbuka: Vipengele vinavyofafanuliwa katika makala haya vinapatikana kupitia kivinjari.

Muziki wa Watayarishi ni orodha inayokua ya muziki wenye ubora wa juu ambayo watayarishi wanaweza kutumia kwenye video bila kupoteza uwezo wa kuchuma mapato. Baadhi ya nyimbo zinaweza kupewa leseni mapema, hali inayowaruhusu watayarishi kudumisha uwezo kamili wa kuchuma mapato. Nyimbo nyingine zinaweza kutimiza masharti ya kugawa mapato na wamiliki wa haki za wimbo.

Ili uanze kutumia Muziki wa Watayarishi, tazama video hii:

Muziki wa Watayarishi

Kufungua Muziki wa Watayarishi

Kipengele cha Muziki wa Watayarishi kinapatikana kwenye Studio ya YouTube. Ili ufungue Muziki wa Watayarishi:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube kwenye kivinjari.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Muziki wa Watayarishi.

Kutafuta na kutazama vionjo vya nyimbo

Kuna njia nyingi za kutafuta nyimbo unazopenda kwenye Muziki wa Watayarishi:

  • Kuvinjari nyimbo zinazoangaziwa kwenye Ukurasa wa Kwanza
  • Kuvinjari nyimbo katika aina kama vile aina na hisia
  • Kutafuta wimbo au msanii mahususi
  • Kutafuta nyimbo zinazoweza kupewa leseni au zinazotimiza masharti ya kugawa mapato

Unapovinjari, unaweza kutazama vionjo vya nyimbo ili vikusaidie kuamua ikiwa zinafaa kwa maudhui yako. Unaweza kupakua vionjo vya baadhi ya nyimbo zinazoweza kupewa leseni ili uhakikishe kuwa wimbo unafaa video yako kabla ya kuupea leseni. Kumbuka kuwa huwezi kupakua nyimbo zilizotiwa alama kuwa zinastahiki ugavi wa mapato .

Unaweza pia kukagua maelezo ya matumizi ya wimbo ili ufahamu jinsi unavyoweza kutumia wimbo kabla ya kuutumia kwenye video yako. Pata maelezo zaidi kuhusu kutafuta na kutazama vionjo vya nyimbo.

Kuhifadhi na kudhibiti nyimbo

Unapopata wimbo unaopenda, unaweza kuuhifadhi kwenye maktaba yako. Kwenye ukurasa wa Maktaba yako, unaweza kutazama, kuchuja na kupanga orodha ya nyimbo ulizohifadhi, ulizopakua na ulizopea leseni. Pata maelezo zaidi kuhusu kuhifadhi na kudhibiti nyimbo.

Kupata leseni

Ukipata wimbo unaoweza kupewa leseni ambao ungependa kuutumia, unaweza kupata leseni moja kwa moja kwenye Muziki wa Watayarishi au unapopakia video inayotumia wimbo huo.

Unapopea wimbo leseni, unahifadhi uwezo kamili wa kuchuma mapato kwenye video yako inayotumia wimbo huo. Kumbuka kuwa nyimbo zinazoweza kupewa leseni zinaweza pia kustahiki kugawa mapato ikiwa matumizi yako ya wimbo yanatimiza masharti ya matumizi ya ugavi wa mapato. Pata maelezo zaidi kuhusu utoaji leseni.

Kugawa mapato

Unapotumia nyimbo zinazostahiki ugavi wa mapato , unagawa mapato ya video na wenye hakimiliki, mradi tu video yako inatimiza masharti ya ugavi wa mapato. Baadhi za nyimbo zinazoweza kupewa leseni zinaweza pia kustahiki kugawa mapato ikiwa video yako inatimiza masharti ya ugavi wa mapato. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ugavi wa mapato hufanya kazi.

Pata maelezo zaidi

Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu utoaji leseni wa nyimbo, kugawa mapato na wenye hakimiliki na jinsi ya kutumia kipengele cha Muziki wa Watayarishi katika Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kipengele chetu cha Muziki wa Watayarishi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7385757238777870490
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false