Kukata rufaa dhidi ya mipaka ya umri kwenye video yako

Mwongozo wetu wa Jumuiya hubainisha maudhui yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye YouTube. Ni kanuni husika ambazo kila video sharti izingatie. Video inapokiuka mwongozo huu, tunaiondoa. Baadhi ya video hazikiuki sera zetu, lakini huenda haziwafai watazamaji wenye umri wa chini ya miaka 18. Tunawekea video hizi mipaka ya umri. Ili kubaini ikiwa video inapaswa kuwekewa mipaka ya umri, tunazingatia masuala kama vile:

  • Vurugu
  • Picha za kutisha
  • Maudhui ya kuchochea ngono
  • Uchi
  • Maudhui yanayoonyesha shughuli hatari au haramu

Video inapowekewa mipaka ya umri, skrini ya onyo huonyeshwa kabla ya video kucheza. Watazamaji walio na umri wa miaka 18 au zaidi wanaweza kuitazama. Ili kupunguza uwezekano wa watazamaji kukumbana na video hizi, hazionyeshwi katika sehemu fulani kwenye YouTube. Video zenye mipaka ya umri haziwezi kutazamwa kwenye tovuti nyingi za wahusika wengine. Video hizi zitawarejesha watazamaji kwenye YouTube wanapozicheza.

Kukata rufaa dhidi ya mipaka ya umri kwenye video yako

Ikiwa video yako imewekewa mipaka ya umri, unaweza kukata rufaa dhidi ya mipaka hiyo.

Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
  3. Chagua video iliyo na kizuizi, kisha uguse kizuizi hicho.
  4. Gusa Kagua matatizo.
  5. Gusa dai husika.
  6. Weka sababu yako ya kukata rufaa kisha ubofye Tuma.

Kukata rufaa dhidi ya mipaka ya umri kwenye video yako

Ikiwa video yako imewekewa mipaka ya umri, unaweza kukata rufaa dhidi ya mipaka hiyo.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Maudhui.
  3. Nenda kwenye video ambayo ungependa kukatia rufaa. 
  4. Katika safu wima ya “Vizuizi”, nenda kwenye aina ya vizuizi. Bofya Rufaa
  5. Weka sababu yako ya kukata rufaa. Bofya Tuma.

Kumbuka: Unaweza kukata rufaa mara moja pekee dhidi ya mipaka ya umri kwenye video yako.

Ukishakata rufaa

Timu ya YouTube itakagua ombi lako na kuchukua hatua nyingine ikihitajika.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4877445118520757386
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false